Tiajin Quanjian inayoshiriki Ligi kuu China iliotoa dau la kumsajili mchezaji wa klabu ya Chelsea wamefuta ndoto hio baada ya sheria mpya ya ligi kuu China kutolewa. amesema mmiliki wa klabu hio Shu Yuhui
Shu ameeleza mipango na ndoto za kusajili wachezaji wa timu ya Taifa ya Hispania Costa (28), na washambuliaji wenzake Karim Benzema, Radamel Falcao na Edinson Cavani.
" Hili limebadilisha mipango yetu ya usajili," amesema Shu
Hapo awali timu ilikua na uwezo wa kuchezesha wachezaji wanne (4) wa mataifa mengine na mmoja (1) kutoka Asia.
Shu ameeleza pia jinsi Tianjin ilivyokuwa imewekeza sana mwaka huu kama sheria hii isinge badilishwa.
Falcao (30) Monaco |
Raul Jimenez (25) Benfica |
"Kuhusu ripoti za Costa kwenye mitandao - ni kweli tunataka kumsajili, na tumetoa ofa kwa Cavani na tupo katika majadiliano," amesema Shu
Billionaire Shu aliongeza kwa kusema Costa na mshambuliaji wa PSG, Cavani (29) wangeweza kutia saini ila klabu zao hawakutaka waondoke wakati michuano inaendelea mpaka mwezi Juni.
"Hatukuweza kusubili nusu msimu," aliongeza Shu
"Tunaendelea kusubili na kusumbuka, ila mwisho wa siku tutapata mtu. Tuna mipango ya washambuliaji wengi, na tumetoa ofa kwa Benzema, ila kutokana na sheria kubadilishwa, hatuna msaada."
Tianjin wamepanda Ligi kuu China msimu uliopita, pia wana Kocha kutoka Italia, Fabio Cannavaro
Kocha Mkuu wa Tiajin Quanjian, Fabio Cannavaro (Picha na Getty Images)
Axel Witsel kutoka Belgium hivi karibuni alisajiliwa na Tianjin Quanjian (Picha na getty Images)
TUPE MAONI YAKO KUHUSU USAJILI WA TIMU ZA CHINA KAMA TIANJIN QUANJIAN..
0 comments :
Post a Comment