Siku mbili baada habari kusamba kuwa Jay-Z amepata watoto mapacha, rapa huyo ameonekana siku ya Jumatatu akiwasili katika hospitali iitwayo Ronald Reagan UCLA Medical Center huko Los Angeles, Marekani.
Baba huyo mwenye watoto watatu sasa alifika katika hospitali hiyo akiwa kava T-shirt nyeupe na suruali yenye mstari mweupe pamoja na kuvalia viatu vyeupe.
Chanzo muhimu kilihakikisha siku ya Jumamosi kuwa Beyonce amejifungua watoto mapacha, pia baba yake mzazi, Mathew Knowles, alithibitisha mwenyewe kupitia mtandao wa twitter.
Mapema siku hio Jay Z alionekana katika darasa la Soul Cylcle huko Beverly Hills.
"Alihudhuria darasa lilipokuwa linaaza," alieleza shuhuda. "Alionekana mwenye furaha na nguvu nyingi. aliendelea na darasa vizuri tu. alionekana akifurahia mazoezi. Alivyokuwa mjamzito, Beyonce alikuwa akija darasani na Jay-Z. Leo alikuwa na rafiki yake."
"Wamefika! #Beyonce #twins #Jayz #happybirthday," aliandika, akiambatanisha na picha ya maputo yaliotiwa sign, "Love granddad.'
Mapacha hao wanaungana na dada yao mkubwa Blue Ivy (5).
Beyonce (35) pamoja na mumewe rapa Jay-Z waliweka wazi kuhusu mapacha hao mnamo mwezi February .
0 comments :
Post a Comment