Wiki hii mitandao ya nchini Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na ugomvi Mkubwa kati ya mapacha wawili wanaounda kundi la P Square,Peter na Paul Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezi.
Habari zilichochewa na tweet hii ya kaka yao Mkubwa ambaye pia ni Meneja wao,Jude Okoye
tweet hii iliyotafsiriwa na mitandao hiyo huenda ameachana na kundi hilo.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo aitwaye Bayo Adeta alikanusha Habari hizo wakati akihojiwa na Premium Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo zimetoka wapi.
Kupitia juhudi za BLOG YA VIJANA tuliweza kupata kuona taarifa kutoka kwa mtu wao mwingine wa karibu alisema maneno haya kwa kingereza na pia tafsiri kwa lugha ya kiswahili utaweza kusoma baada ya maneno haya ya kingereza...
Maneno hayo yaliosemwa na mtu wa karibu unaweza kuyasoma kwa kiswahili hapa chini...Tafsiri na (Blog ya Vijana- email- blogyavijana@gmail.com)
"Ndio wamepigana
wiki hii, Peter ameacha alama kwenye jicho la kushoto la Paul, ila ugomvi huo
haukua muda wa mazoezi, Mazoezi gani? Peter amegoma kufanya kitu chochote
kuhusiana na P-Square kwa wiki. Sahau kuhusu kuwepo kwenye harusi ya kaka yake,
ila mambo hayapo vizuri baina yao kwa sasa. Peter anataka kutoka. Amesema Paul
na Jude wanamtenga yeye, Kwamba wakitoa nyimbo 200 basi 199 zitakua nyimbo
ambazo amefanya Paul, mpaka watu wanamuona kama yeye mchezaji ndani ya
P-square. Peter amechukia sana, ni mtu safi sana na rafiki wa watu, Pia
amemtuhumu kaka yake Jude kwa kosa la kutomheshimu mke wake Lola kwa miaka
mingi na amechoka kuendelea kuona hivyo. Hata hivyo Peter amesema kwamba sio tu
Lola ni mkubwa kwa Jude ila pia ni Mjamzito na Jude amekuwa akimkasirisha
mwanamke mjamzito. Kama ulikua makini Jude akuhudhuria harusi yao mwaka jana
hata kama alikua Nigeria. Jude alimuuliza Peter kwanini hakumuoa Lola wakati
mama yao yupo hai. Jude amesema ni mke wake anae msukuma peter na wanatakiwa
kumuombea. Inasemekana hakuna mtu katika familia ya OKoye anampenda Lola na
hawakushinikiza ndoa yao. Makaka hao wamekasirikiana sana, hata mapolisi
wanahusika sasa, wiki mkubwa wa mapolisi au mtu kutoka ofisini alitembelea
nyumbani kwao.
Kitu kibaya
ni kwamba wamemwita wanasheria aje kugawanisha mali zao, wanataka wagawane kila
kitu. Mwanasheria alikua kwao nadhani Alhamisi. Peter alisema hakuna tena kushirikiana
kwa P-Square, Unajua wanamiliki kila kitu pamoja pamoja na nyumba iliopo Omole,
Parkview na Atlanta. Mambo yasipofanyika haraka basi P-square inakaribia kufa.
Najua watu wamekuwa wakiingilia na kuomba sana waelewane, kwamba wao ni kundi
kubwa sana hapa Afrika, hakuna atae faidika kama wakitengana. Nguvu ya wao
kutengeneza pesa ipo kwenye umoja wao.
"Ni jude amabe watu wanamuomba
awapatanishe makaka hao, lakini baada ya alichokiandika twitter hapo jana
inawezekana ndo ikawa mwisho wa P-Square. Jude amejitahidi sana kwa ajili ya
kaka zake mpaka kufikia hatua ya kuacha vitu vingi kwa ajili yao.
Jude
amesimamisha maisha yake binafsi kwa ajili ya kaka zake. Aliuza gari lake
lakwanza ili waweze kushoot video yao yakwanza ila yote hayo yamefikia mwisho
wake kama alivyo andika twitter. Kitu kinachoweza kuweka mambo sawa ni labda maajabu yatoke Jude na Lola waondoe tofauti zao, ila sioni hilo likitokea ”
Source; BLOG YA VIJANA Endelea kupata habari za kina zaidi hapa ili kuwa mwana familia wa Blog hii na kuweza kupata habari punde tu zinapotokea like page yetu ya facebook kwa kubonyeza hapa BLOG YA VIJANA ni bure kabisa
wanawake
ReplyDelete