MBEYA City imemaliza Ligi Kuu Bara kwa kushika nafasi ya tatu na sasa imeanza kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao kwa maana na usajili pamoja na kutengeneza miundombinu yake, likiwamo suala la usafiri kwa kununu basi la kisasa litakalokuwa ‘ndege ya chini’.
Mikakati mingine ya miundombinu hiyo ni kujenga
uwanja wao. Kwa suala la uwanja, inatarajia kuanzisha kazi ya kuujenga
katika eneo la Iwambi mjini Mbeya. Eneo lao limeelezewa kuwa na ukubwa
ekari 15.
Ukija kwenye suala la usafiri ambalo linatarajia
kukamilika muda si mrefu kutoka sasa, klabu hiyo inatarajia kununua basi
jipya la kisasa lenye huduma zote ndani. Basi hilo litakuwa ama Yutong
au Higer.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe,
ameliambia Mwanaspoti kuwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambayo ndiyo
mmiliki wa timu hiyo, imeshatangaza tenda kwa kampuni mbalimbali
zinazouza magari baada ya kuweka wazi sifa za basi wanalolihitaji.
“Tulitangaza mara ya kwanza, hakukuwa na kampuni
iliyojitokeza, tukarudia ndipo kampuni tatu zimejitokeza na hivyo
itapendekezwa kampuni moja kulingana na makubaliano yatakayofanyika,”
alisema Kimbe.
“Tupo katika hatua za mwisho za ununuzi wa basi la timu, tutahitaji moja lenye hadhi tunayoitaka, fedha zipo.”
Source.. Mwanaspoti
Source.. Mwanaspoti
0 comments :
Post a Comment