.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

FRIENDS RAGERS KUPAMBANA NA RUVU SHOOTING LEO....6/9/2013

TIMU ya soka ya Friends Rangers ya Dar es Salaam, leo inaingia dimbani kuvaana na Ruvu Shooting ya Pwani, katika mchezo wao wa kirafiki uliopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Mabatini.

Friends Rangers itacheza mchezo huo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja la Kwanza inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 14 mwaka huu.

Katika ligi hiyo ya Daraja la Kwanza timu hiyo ambayo ni ngeni katika michuano hiyo itaanza ligi kwa kuvaana na Ndanda FC ya Mtwara, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaiona.

Akizungmza Dar es Salaam jana, Asha Kigundula ambaye ni Ofisa Habari wa Friends Rangers alisema lengo la mechi hiyo kukipa mazoezi kikosi chao kinachojipanga kupanda daraja hadi Ligi Kuu.

Alisema lengo leo kubwa ni kuimarisha kikosi hicho ili kiweze kufanya vema kwenye ligi hiyo na hatimaye kupanda kushiri ligi kuu msimu ujao.

Alisema mbali na mechi ya leo timu hiyo imejipanga kucheza mechi nyingine tatu za kirafiki kabla ya kuanza safari yao ya kuelekea mkoani Mtwara kwenye mechi kati yao dhidi ya wapinzani wao Ndanda.

"Sio mechi hii tu, tumejipanga kupata mechi kama tatu za kirafiki, lengo likiwa ni kuendelea kujipanga kimashindano na kufikia malengo tuliyojiwekea ya kupanda Daraja kwenda Ligi Kuu," alisema KIgundula.

Timu hiyo yenye maskani yake Magomeni, Kagera Dar es Salaam, ipo katika Wilaya ya Kinondoni,ikiwa imesajili wachezaji wengi vijana na wachezaji wachache wenye uzoefu wa Ligi Kuu ambao wamewahi kucheza katika timu kubwa za hapa nchini.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad