Janjaro msanii kutoka Arusha lakini
makazi yake yapo Dar amefunguka na DJCHOKAblog kuwa hajafukuzwa na Ostaz
Juma Namusoma kwenye kampuni yake ya Mtanashati bali amejitoa mwenyewe
kwa hiari yake. Janjaro amesema amechoka na matendo tu ya Ostaz na
alikuwa tu akiyavumilia lakini kwa sasa ameshakuwa mkubwa so nataka
nikae kivyangu vyangu nifanye mambo yangu kama wasanii wengine ambao
hawana meneja na wanafanya poa. Namnukuu Janjaro akisema....
"Najua yatasemwa mengi kutoka kwa Ostaz Juma ila mimi ndio uwamuzi wangu, kuna watu wanasema sina utovu wa nidhamu lakini hao watakuwa wananijua sasa hivi hawajanifuatilia kutoka nyuma. Hata mtoto mdogo atakuwa mtundu ila akiwa mkubwa hunyooka na kuwa mtoto mzuri sasa nimekuwa mkubwa na kupelekwa pelekwa tena sitaki, kwa maelezo zaidi Ostaz Juma aongee na wazazi wangu asiongee na mimi"

0 comments :
Post a Comment