.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

VITUO VYA MWENGE NA UBUNGO KUHAMISHWA JIJINI DAR



Vituo vya daladala vya Ubungo na Mwenge vinahamishwa kupisha Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART), ambao miundombinu yake inaendelea kujengwa.

Ofisa Habari wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera amekaririwa akisema yafuatayo:-
Kituo cha Ubungo kitahamishiwa nyuma ya jengo la Mawasiliano lililopo Barabara ya Sam Nujoma.
Kituo cha Mwenge, kitatumika kwa ajili ya kushusha abiria pekee.
Magari ya Mwenge, yatakuwa na uamuzi wa ama kuishia kwenye stendi ya Makumbusho au kwenda hadi kituo hicho kitakachohudumia magari ya Ubungo (kilichoko Mawasiliano).
Wakati wowote kuanzia sasa vituo hivyo, vitabomolewa kupisha mradi huo.

Kuhusu hatua zinazochukuliwa na manispaa, kuwezesha wafanyabiashara ndogo kupata maeneo ya kuendesha shughuli zao alisema, hakutakuwa na mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza bidhaa zozote katika kituo kipya, kama ilivyo sasa kwa vile hakutakuwa na nafasi kutokana na  eneo lote kutumika kwa ajili ya barabara.

Akasema kwa hali hiyo wafanyabiashara watalazimika kwenda katika maeneo waliyopangiwa: “ Kwa hiyo ni bora wakaanza kujiondosha wenyewe mapema kabla hatua ya kuondolewa na ujenzi kuwafikia,” alisema na kuongeza kuwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kazi hiyo yapo katika masoko mbalimbali likiwemo la Kijitonyama.

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad