Early life
Muigizaji huyu alizaliwa katika hospitali ya Agha khan, tarehe 19 mwezi wa tisa na ni mtoto wa pili katika familia ya mzee bagenzi. Kwa upande wa elimu yake, mwanadada huyu amesoma mpka akidato cha tano na kuamua kusimama kwa muda kutokana na matatizo binafsi kabla ya kujiingiza kwenye sanaa ya uigizaji.Career
Rayuu alianza kuigiza toka akiwa shule ya msingi ila kuanza kuonekana rasmi kwenye luninga ilikuwa ni baada ya kujiunga na kundi la sanaa la kaole lililokuwa likirusha vipindi vyake vya maigizo kupitia kituo cha ITV kundi ambalo aliweza kupata nafasi ya kujiunga nalo kupitia kwa marehemu mzee kipara ambaye Rayuu anasema alimfuata walipokuwa wakiigiza na kundi hilo maeneo ya nyumbani kwao na kumuomba ajiunge nalo ndipo mzee kipara alipompeleka kwenye kundi hilo rasmi kwa mara ya kwanza. Baada ya kaole rayuu alipata nafasi ya kuigiza kwenye filamu ya Vicenti kigosi ama Ray (The image) na baadae akafanya filamu ya Trinity kabla ya kupumzika kwenye filamu kwa muda. Vyombo vya habari Mwanadada Rayuu alipata kuwa kwenye vichwa vingi vya habari kipindi Fulani baada ya picha zake kadhaa za alizopiga akiwa hana nguo kusambaa kwenye mitandao lakini mara nyingi mrembo huyu anasema hiyo siyo kweli kwani picha hizo hazikuwa na maana hiyo kama watu walivyozichukulia.Ugomvi na mwigizaji Sintah Mwanadada huyu pia amekuwa kweny ugomvi “beef” wa muda mrefu na mwanadada Sintah ambao chanzo chake mpaka leo huwa hakipo wazi ingawa yeye mwenyewe husema kuwa sintah ndo anayetafuta ugomvi naye Maisha binafsi Katika mahojiano naye Rayuu huwa anasema yeye ni mtu wa kupenda kushinda ndani na kuangalia filamu siku nzima kama hayupo kazini.
0 comments :
Post a Comment