.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

BREAKING NEWS: MWANDISHI WA HABARI WA ITV&RADIO ONE UFOO SARO AMEPIGWA RISASI , MAMA YAKE MZAZI KUWAWA PAPO HAPO

 
Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata hivi punde katika habari mpasuko ya Radio One kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwamba, Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa ITV na Radio One Stereo Ufoo Saro amejeruhiwa kwa kupigwa risasi baada ya kuvamiwa na mtu asiyefahamika nyumbani kwake Kibamba Kinondoni Jijini Dar es salaam.



Aidha mvamizi huyo alimuua mama yake Ufoo papo hapo na yeye mwenyewe kujiua kwa risasi, 


Aidha anayedhaniwa kufanya mauaji hoyo ya kutisha  ni mume au mchumba wa mwandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro na yeye mwenyewe kujiua.
akizungumza na mtandao huu kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni kamanda Wambura amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda wambura ameongeza kuwa mwanaume huyo anafanya kazi umoja wa mataifa UN huko sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani (japo kwa habari za mtaani zinasema mtu huyo ni mwanajeshi ila bado hazijathibitishwa)
Kamanda Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga Ufoo Saro risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad