Mtanzania, Malkia Kassu ( wa tatu toka kushoto) akiwa na washindi wenzake – wote wamevalia taji na kubeba vikombe vya ushindi. Mashindano ya 2013 yalifanyika London Jumamosi Novemba 26 na kwa mara ya kwanza yalikuwa na mshiriki toka Tanzania.
Malkia Kassu ( jina la kuzaliwa Mulki Kassu Miraj) alichaguliwa malkia wa Tanzania na bara zima la Afrika.
Wateuzi wa ushindi huo hawakuangalia tu sura, bali tabia, fikra, hamasa na msimamo wa kimaendeleo wa mhusika ambapo washindani walitoka mataifa mbalimbali duniani.
“Ninataka kuiwakilisha nchi yangu na kuwasaidia wenye maisha magumu, niifanye dunia iwe mahali pazuri zaidi. Nafahamu si kazi rahisi ila nina hakika kila mmoja wetu akijumuika na mwenzake mabadiliko mema zaidi yatafanyika. Tanzania ni nchi ya amani na ninaamini amani na mapenzi vyaweza kuongezeka katika jumuiya zetu.” – Kassu
0 comments :
Post a Comment