Edward Lowassa.
Katika hali isiyo ya
kawaida, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, ambaye huongea kwa nadra bungeni, Edward
Lowassa leo amenguruma na kutaka taifa kuacha kuweka vipaumbele vingi
visivyotekelezeka kwa wakati.
Alitaka serikali kuweka
nguvu katika vipengele vichache vya msingi kama ajira, afya, elimu na
miundombinu.
Aliwapongeza mawaziri John Magufuli kwa kuimarisha barabara na Dk. Harrison Mwakyembe kwa kubuni mbinu za kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, alizosema zinachangia kuharibu uchumi kwani watu wengi wanakaa barabarani badala ya kufanya kazi.

0 comments :
Post a Comment