Afisa
Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa
Bodi ya ushauri wa Umoja wa Afrika ya kupambana na Rushwa yaani African
Union Advisory Board on Corruption (AUABC) na Tamasha la wasanii lenye
lengo la kufikisha ujumbe juu ya Madhara ya Rushwa kwenye Jamii, Kati
kati ni Emmanuel Atenga toka (AUABC) na Stephane Ndilimbaye toka AUABC.
Na.Mwandishi wetu
TAASISI
YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Bodi ya
Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) na
Megamark Ltd wameandaa tamasha kubwa litakalowashirikisha wasanii mbali
mbali toka Tanzania, Kenya na Uganda katika kuadhimisha miaka 10 tangu
bodi hiyo ya Afrika katika maswala ya Rushwa kuanzishwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark ltd, Chedi Ngulu amesema kuwa lengo la
tamasha hilo ni kufikisha ujumbe kwa umma juu ya kupambana na Rushwa na
kuelezea madhara ya Rushwa kwenye jamii na nchi kwa ujumla.
Bw. Emmanuel
Atenga (wa pili kushoto) kutoka na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika
katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) akizungumza
na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo litakalofanyika tarehe 7
mwezi ujao katika viwanja vya General Tyre Arusha. Kulia ni mmoja wa
wasanii wataoimba kwenye Tamasha hilo Fid Q na wa pili kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu na kushoto ni Stephane
Ndilimbaye kutoka AUABC.
“Muziki
upo katika asili ya waafrika na umekuwa ukitumika kuburudisha lakini
zaidi kufikisha ujumbe wenye kujenga na kurekebisha jamii (Hadhira) iwe
ni nyimbo, kughani ambayo tunatambua kwa njia ya Rap na ngoma za asili,
lakini tumechagua muziki kama njia rahisi ya kufikisha ujumbe hasa kwa
vijana kuhusu madhara ya Rushwa,” amesema Ngulu.
Amesema
kuwa katika tamasha hilo nyimbo mbalimbali zitaimbwa katika kuelezea
matatizo ya Rushwa kwenye jamii na hasa kuelimisha vijana umuhimu wa
kukataa Rushwa kwa sababu vijana ndio nguvu kazi ya taifa na asilimia 75
ya watu nchini ni vijana.
“kwa
mantiki hii, tumeandaa onyesho lenye anuani isemayo “Rushwa sio”
ikimaanisha rushwa haina manufaa na ni yenye kutakiwa kupigwa vita kwa
gharama yoyote ile,”
Msanii Fid Q akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo.
“Onyesho
hili litafanyika Arusha tarehe 7 mwezi wa kumi na mbili katika viwanja
vya General Tyre kuanzia saa saba na nusu mpaka saa kumi na mbili jioni
na litahusisha wasanii wenye kukubalika na jamii,” alisisitiza
Kwa
upande wake, Emmanuel Atenga toka Kitengo cha Mawasiliano (AUABC)
amesema Board hiyo ya Umoja wa Afrika ya kupambana na rushwa imepata
mafanikio kwa kuanzisha vitengo vya ufatiliaji kwa wanachama wa Umoja wa
Afrika wenye lengo la kusaidiana katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Amesema
mapambano dhidi ya rushwa Afrika yanahitaji nguvu ya pamoja kwa
ksuhirikisha jamii wakiwemo wasanii katika kuhamasisha mapambano ya
kukataa Rushwa kwenye ngazi zote ndani ya nchi na bara zima la Afrika.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
0 comments :
Post a Comment