§ MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM SAIDI MBOYA,
MIAKA 36, MKAZI WA DSM ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU
HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIFAHAMIKA JINA KWA MUJIBU WA HATI YAKE YA
KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 KUTOKA DSM KUELEKEALILONGWE NCHINI MALAWI.
§ MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI AKIWA KATIKA BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRIT.319 BLZ AINA YA NISSAN KWA MUJIBU WA TIKETI YAKE ILIYOKUWA NA JINA LA KASSIM MUECK MICHAEL, AKIWA
NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS,T-SHIRT MOJA NYEUSI,RABA
JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU,MKATE MMOJA ,MKOBA MDOGO WA KIUNONI,VACCINATION
CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RANDI MBILI SARAFU ZA AFRIKA
KUSINI NA MIFUKO SITA YA RAMBO RANGI NYEUSI.
§ AWALI BASI HILO BAADA YA KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA
ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU
ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA GARI
HUKU HALI YAKE YA KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.
§ WAHUSIKA
WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA
NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO
KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.
§ KUFUATIA
DALILI ALIZOKUWA NAZO KABLA YA KUFARIKI ILIBIDI MWILI WA MAREHEMU
USAFIRISHWE HADI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO
ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.
§ TARATIBU
ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA DAWA. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.
§ KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA BIASHARA
HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA KWANI SIO TU NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI
BALI PIA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA WAKAZI WA
MBEYA NA TANZANIA KWA JUMLA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI
YA UTAMBUZI WA MWILI WA MAREHEMU.
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
0 comments :
Post a Comment