Juzi
na jana kulikuwa na habari katika gazeti na mitandao mingi kuwa Wastara
na Bond Bin Suleiman ni wapenzi na wamekuwa wakifanya siri sana huo
uhusiano wao. Habari ambazo zilinukuu chanzo
kimoja zilieanda mbali zaidi zikisema huenda Bond ana tabia ya kufanya
mapenzi na mwanamke kotekote kwani aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Lulu
Semagongo(Anti Lulu) alidaiwa kuwahi kukaririwa akisema kuwa anapenda
sana kufanya mapenzi kinyume na maumbile na hawezi kuacha tabia hiyo.
Baada
ya habari hizo kusambaa ilibidi blog yetu kuwatafuta mastaa hao wawili
na wa kwanza kupatikana alikuwa ni Wastara na alikana kuwa katika penzi
na Bond ila alisema wanafanya kazi pamoja kwani kwasasa wanashuti
filamu mpya ya Bond inaitwa Uaminifu Dhaifu. Aliongeza kwa kusema kuwa
Bond ni kama kaka yake. "sina mahusiano na Bond zaidi ya kikazi tu na
zile picha zote ambazo unaziona ni wakati tupo location tukiandaa filamu
yake inaitwa Uaminifu Dhaifu, huo ndiyo ukweli, bora mume wangu
angekuwepo haya yote yasingetokea
Baada
ya hapo ilibidi kumgeukia Bond ambaye yupo location wakimalizia filamu
hiyo na alipoelezewa hayo alisema hana uhusiano wa kimapenzi na Wastara
na picha zinazodaiwa kuwa ni wapenzi ni za filamu mpya ambayo tuliweka
hata hapa katika blog yetu, alisema kuwa huyo Anti Lulu anatafuta
kuandikwa tu kwenye magazeti ndiyo maana anatoa habari hizo zisizo za
kweli ili kujipatia umaarufu "Sio kweli ni picha za kazi tu ambazo hata
wewe nilikutumia magazeti yanazigeuza, Lulu achana nae anatafuta
kuandikwa, tulishachana kitambo wala hatuna mawasiliano.
0 comments :
Post a Comment