
Benard Paul aka Ben Pol amefunguka rasmi kuhusu picha zake zilizozua utata wiki iliyopita
Ben Pol amedai kuwa amefanikiwa kwa kile alichokifanya (Art Work) kutokana na mashabiki walivyoipokea
. "Mimi kama msanii nafanya sanaa ustadi wa kuonesha mawazo kwa jamii, kwa hadhira, kwa mshabiki nilitaka kuonesha mchoro/taswira ya mtu aliyetekwa nilikuwa naitaka ile feeling ya kutekwa, kwa hiyo nisingeweza kuweka uhuru siwezi kuweka hali yoyote ya haki au privacy kwenye ile picha. Kwahiyo mkanganyiko ulioletwa kwangu mimi nimefanikiwa kama sanaa (Artwork)" alisema @iambenpol .
.
Vile vile Ben Pol ameongeza kwa kusema kuwa mama yake alishindwa kulala baada ya kuziona picha hizo mtandaoni.
Ben Pol akiwa na Mama yake Mzazi
" Mama yangu ameshindwa kulala Ijumaa, nimeipost ile picha Alhamis usiku Ijumaa nikaweka nyingine mzee kanipogia simu kama mara 6 nimepokea ananiambia 'vipi nimeona picha umefungwa makamba vipi uko wapi'?" aliongeza
Moja ya wadau wakubwa wa muziki nchini ambae hakuwa na shaka juu ya kile alichokifanya Ben Pol ni P Funk Majani @majani187 ambapo alisifia kitu alichokifanya kwa kusema "mbona kama ni cover, Hii sio kiki ni Good Art Work" alifunguka majani

0 comments :
Post a Comment