Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Sokoine pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri karika msomo
mbalimbali wanaotarajiwa kufanya mahafali yao leo tarehe 29, Novemba 2013 katika
chuo hicho. Waziri Nchimbi alitoa vyeti
na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika msomo mbalimbali chuoni hapo. Kulia
ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Gerald Monela. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi
la Magereza (CGP) John Minja na Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Profesa Peter
Gillah. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpa cheti mwanafunzi Nuru Ally
aliyefanya vizuri kuliko wanafunzi wote katika somo la Development Studies
katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kilichopo mjini Morogoro. Mwanafunzi
huyo pia alikabidhiwa zawadi ya Shilingi 50,000. Kushoto ni Makamu Mkuu wa
Chuo-Taaluma SUA, Profesa Peter Gillah. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wapili kushoto aliyevaa tai) wakiwa katika
picha ya pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja na
wanafunzi waliofanya vizuri karika msomo mbalimbali wanaotarajiwa kufanya
mahafali yao kesho tarehe 29, Novemba 2013 katika chuo hicho. Waziri Nchimbi alitoa vyeti na zawadi kwa
wanafunzi waliofanya vizuri katika msomo mbalimbali chuoni hapo. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments :
Post a Comment