.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

YANGA KUPANDA KILELENI LIGI KUU

Kikosi-cha-Yanga_0e4b9.jpg

MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans wanaonolewa na kocha Mholanzi, Ernie Brands akisaidiwa na Mtanzania Fredy Ferlicx Minziro Katalaiya Majeshi Baba Isaya wanaingia kibaruani leo hii uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kukabiliana na wapiga kwata wa JKT Ruvu kutoka mkaoani Pwani.
Afisa habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto ameuambia mtandao waFULLSHANGWE kuwa maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo yamekamilika na wachezaji wapo katika hali nzuri ya kutafuta ushindi wa tatu mfululizo..
"Kama iilivyo kawaida, Yanga ni timu inayocheza soka safi, tumejiandaa vizuri kuchukua pointi tatu muhimu leo hii na kupanda kileleni mwa ligi kuu soka Tanzania bara kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka huu kuanza". Alisema Kizuguto.
Kizuguto alisema kikosi cha Yanga kina wachezaji wengi wenye uwezo na leo hii ni chaguo la kocha Brandts kuamua nani anaanza.(P.T)
"Nawaombe mashabiki wa Yanga, timu ya wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia soka safi la kikosi chao kilichoimarika kila idara, tupo kamili gado". Alisema Kizuguto.
Mara baada ya ushindi wa pili mfululizo wa mabao 3-0 dhidi ya Rhino Rangers na Mgambo Shooting kikosi cha mholanzi Ernie Brandts kimeendelea kuimarika na safu ya ulinzi ikicheza michezo miwili pasipo kuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Mpaka sasa Young Africans inashika nafasi ya tatu ikiwa na ponti 22 pointi 1 nyuma ya timu zinaongoza mbili za Azam FC na Mbeya City zote zikiwa na pointi 23 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Young Africans inahitaji pointi tatu muhimu katika mchezo huo wa leo dhidi ya JKT Ruvu ili iweze kujikita kileleni na kukalia kiti cha uongozi wa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 25 ambazo zitaweza kufikiwa na timu mbili tu za Azam FC na Mbeya City ambazo zitachezwa mwishoni mwa wiki.
Timu iliingia kambini juzi jioni katika hostel zilizopo makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwa vijana wa Jagwani kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi na kupata pointi tatu muhimu.
Katika mchezo wa leo Young Africans itakosa huduma ya wachezaji wake David Luhende na Nizar Khalfani ambao ni majeruhi huku kiungo Haruna Niyonzima akiukosa mchezo huo kutokana na kuwa nchini Rwanda alipokwenda kushugulikia matatizo ya kifamilia.
Nao JKT Ruvu kupitia kwa kocha msaidizi, Geryson Haule wametamba kupambana mwanzo mwisho kuhakikisha wanaibuka na ushindi mbele ya Yanga.
"Yanga ni bora, hilo halina ubishi. Lakini leo hii tutakwepa kuwa ngazi ya kuchukulia pointi tatu na kuwapa nafasi ya kuongoza ligi". Alisema Haule.
Kocha huyo alisema kikosi chao awali kilikuwa kinasumbuliwa na majeruhi, lakini sasa kimekuwa sawa baada ya mabeki wake wa kati kupona na kurejea uwanjani.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad