Siku moja
baada ya kupokea kipigo cha kihistoria cha 5-0 kutoka kwa Liverpool
wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, klabu ya Tottenham Hotspur
imemtimua kocha mkuu wa timu hiyo Andre Villas Boas.
Tottenham
ambao walikuwa ndio timu iliyotumia fedha nyingi kufanya usajili wakati
wa dirisha la usajili, wakitumia zaidi ya paundi millioni 100, wameanza
vibaya msimu huu na hivyo kufikia maamuzi ya kumtimua AVB ambaye
alijiunga na timu hiyo miezi takribani 18 iliyopita.
Majina
ya Luis Enrique na Fabio Capello yameanza kutajwa kuja White Hart Lane
kuchukua nafasi inayoachwa wazi na kocha huyo wa zamani wa Chelsea na
Porto
0 comments :
Post a Comment