Kundi lakwanza la watu zaidi ya 10,000 wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji wamepokelewa katika mji wa Munich (Ujerumani) baada ya safari ndefu kupitia Hungary na Austria.
Wananchi wa Ujerumani wamejitokeza kuwakaribisha na kuwapa zawadi kama pipi wakati wahamiaji 450 walipowasili na usafiri wa treni.
Mapema wiki hii picha mbali mbali za kusikitisha zikionesha watoto wakiwa wamekufa pembezoni mwa bahari zilisamba kutokea Budapest wakati Hungary ilipowazuia kuendelea na safari ya kuelezea Austria.
Wahamiaji wengi walikata kuwekwa kwenye kambi nchini Hungary ili kusajiliwa huku wakisisitiza kuwa wanataka kuendelea na safari ili wafike Ujerumani au Austria.
Makundi ya watu walivunja na kuweza kupita, kisha kuanza kutembea umbali wa kilomita 175 (Mile 108) kuelekea border ya Austria, wengi wao wakiwa na watoto.
Safari hio ilianza mchana wa siku ya Ijumaa kutokea kituo cha treni huko Budapest.
Giza lilivyokuwa linazidi kutanda huku bado wakiwa barabarani na baridi likiwa kali, Hungary kuhofia usalama iliwabidi watume mabasi kuwabeba na kufikishwa katika border ya Austria, kisha mabasi hayo yalitumika kuwabeba wahamiaji wengine walioweka kambi katika kituo cha treni cha Budapest.
Mpaka kuimaliza Jumamosi inakadiliwa Hungary kupitia border ya Austria wameokea wahamiaji 10000
Wahamiaji wakiingia kwenye basi litakalo wapeleka Ujerumani au Austria
Wakizungumza na BBC Austria wamesema hawato weka kizuizi cha idadi ya wahamiaji watakao kuwa wanapita kwenye border, Msemaji wa waziri wa mambo ya ndani alisema kuwa nchi inakabiliwa na watu kutoka miji yenye machafuko.
Huko Chancellor Angela Merkel amesema Ujerumani inaweza kumudu wageni wapya, bila kuongeza ushuru au kuongeza budget.
Wapo ambao wanatembea kuelekea kwenye Border ya Austria umbali wa kilimita 175 huku wakitarajia kukutana na mabasi yatakayo wafikisha Austria kisha kupelekwa Viena.
0 comments :
Post a Comment