.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

HII NI FUNGA MWAKA!!!! MAKAHABA WANASWA NA WATEJA WAO....WADAI WANASAKA PESA YA SIKUKUU...TAZAMA MAPICHA ZAIDI YA 12 HAPA....LAANA TUPU


AISEEE! Yameshuhudiwa matukio mengi ya kamatakamata ya dadapoa kwa mwaka 2013 lakini hili ni funga mwaka. Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kwa kolabo na polisi, safari hii imefumua madanguro mengi yaliyojificha vichochoroni na kwenye nyumba za kulala wageni na kuibuka na mambo mengi ya kushangaza.


Katika oparesheni hiyo maalum iliyofanywa na OFM na polisi wa Kituo cha Buguruni, Dar, usiku mnene, mwanzoni mwa wiki hii, ilifanikiwa kuwanasa akina dada wanaouza miili katika maeneo mbalimbali wakiwa na wateja wao ambapo baadhi yao walitiwa mbaroni.



MAENEO MENGINE

Ukiachilia mbali sehemu za madanguro hayo, OFM ilitonywa kuwepo kwa baadhi ya gesti zinazotumiwa na wanawake hao kama madanguro kwa kuingiza na kubadili wanaume asubuhi, mchana na usiku.


Oparesheni hiyo ilisafisha maeneo ya Buguruni ambayo ni korofi kwa biashara hiyo haramu ambapo baadhi yao walidai kuwa wapo kwenye mishemishe za kusaka fedha kwa ajili ya sikukuu ijayo ya Krismasi.



MENGI YABAINIKA

Katika upelelezi wetu, baadhi ya wanawake walionaswa kwenye sekeseke hilo, ni wachumba na wake za watu.


Baadhi ya watu waliokuwa karibu na maeneo hayo, walisema imekuwa ni kero kwao kwani uwepo wa wanawake hao maeneo hayo huleta picha mbaya kwa jamii hasa watoto.



“Safi kabisa, nalipongeza sana jeshi la polisi na OFM kuweza kuyabaini na kuyafanyia kazi maovu haya, watoto wetu wamekuwa wakishuhudia uchafu mwingi sana,” alisikika mama mmoja wa makamo.


MACHANGUDOA HAWA HAPA!

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyuso za huzuni, baadhi ya wanawake walionaswa walikiri kuwa wachumba na wake za watu ila kutokana na ugumu wa maisha wanalazimika kujiingiza kwenye biashara hiyo.


“Jamani naombeni sana mniache, niko hapa si kwa kupenda kwani ugumu wa maisha ndiyo chanzo, mume wangu kwa sasa hayupo, tafadhalini jamani,” alisema mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la mama Batuli.

Wengine walisema si wake za watu lakini wapo maeneo hayo kusaka fedha za kujinasua na ukata kutokana na ukosefu wa ajira hasa kuelekea kwenye kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.




WATEJA WAO SASA

Waandishi wetu waliendelea na upekuzi kwa kuwapeleleza wanaume wateja walionaswa nao kwa kuwauliza kulikoni wafanye hivyo wakati mitaani kumejaa wanawake wengi wastaarabu ambapo walifunguka kuwa chanzo ni matatizo ya kindoa.



POLISI NA MSIMAMO WAO

Hata hivyo, jeshi la polisi kupitia Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi Buguruni (OCD), Lucy Kakuru alisisitiza kuwa wataendelea kupambana na biashara hiyo haramu hadi suala hilo liishe maeneo hayo.


Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad