Add caption |
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ leo amemuonyesha Emmanuel Okwi fulana yenye maandishi yanayomnanga.
Kaburu
aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Simba kabla ya kujiuzulu miezi kadhaa
iliyopita, alimuonyesha Okwi jezi hiyo aliyokuwa amevaa.
Jezi
hiyo ilikuwa imeandikwa, “I always remember Mafisango, who is Okwi?”
(Kila mara namkumbuka Mafisango, kwani Okwi ndiyo nani?).
Okwi alipokwenda kuwasalimia upande wa benchi la Simba, Kaburu alimuonyesha Okwi maandishi hayo, akaonyesha kushtuka lakini baadaye wakakumbatiana.
Okwi
alikuwa katika kikosi kilichoifunga Yanga mabao 5-0 pamoja na Mutesa
Mafisango ambaye alifariki dunia wiki chache baadaye kwa ajali ya gari
jijini Dar
About feisal pinto
Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
0 comments :
Post a Comment