Chacha Makenge (36) akiwa amepozi ndani ya chumba chake 'handaki'.
Akitoka katika handaki lake.
Chacha katika pozi nje ya handaki lake. |
Na Makongoro Oging’/GPL
DUNIA haiishi vituko! Chacha Makenge (36) mzaliwa wa Kijiji cha
Kisangula, Mtukula, Serengeti mkoani Mara anaishi jijini Dar lakini
ndani ya handaki aliloligeuza chumba kwa miaka minne sasa, ni ajabu
lakini ni kweli.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
hivi karibuni nje ya handaki hilo lililopo mita chache kutoka majengo
ya biashara ya Mlimani City, Makenge alisema alichukua uamuzi huo baada
ya rafiki yake (jina linahifadhiwa) kumchomea nyumba na kuteketeza
samani zote.
“Ilikuwa mwaka 2009 mwanzoni rafiki
yangu huyo ndiye alinipa sehemu ya kiwanja chake nijenge nyumba. Nikawa
naishi hapo huku nikiendelea na shughuli zangu za kila siku.
“Siku moja akabadili mawazo, akanitaka nihame katika eneo lake bila kunipa sababu, nilimwomba anipe muda nitafute pa kwenda.
“Julai 2009 akaja na polisi, akanikamata na kunipeleka Kituo cha Polisi cha Stakishari, nilipowauliza kosa langu, hawakunieleza.
“Baada ya siku mbili majirani walikuja kuniona na kuniambia kwamba
nyumba yangu imechomwa moto na kila kitu kilichokuwa ndani kimeteketea,
aliyefanya hivyo ni rafiki yangu. Nilijisikia vibaya sana.
“Siku iliyofuata majirani walikuja tena
kituoni wakaniwekea dhamana. Nilipofika kwangu nilikuta majivu tu,
iliniuma sana, nililia lakini sikupata ufumbuzi. Kwa vile nilikuwa sina
pa kwenda ilibidi niwe nalala palepale nilipochomewa nyumba nikisaidiwa
chakula na majirani.
“Siku iliyofuata, saa nne usiku
nilivamiwa na watu wanne, wakiwa na mapanga na marungu, nilipambana nao
mpaka wakaondoka. Kesho yake nilikwenda kwa mwenyekiti wetu wa serikali
ya mtaa, Jumanne Malima kumweleza yaliyonipata, alisikitika,
akaniandikia barua kwenda Polisi Stakishari.
“Nilipofika
kituoni sikusikilizwa, badala yake walinikamata tena na kuniweka ndani
wakidai kwamba nimefunguliwa kesi ya kumjeruhi mtu kwa panga.
Hawakukubali niwekewe dhamana.
“Julai
31, 2009 nilifikishwa Mahakama ya Mwanzo Ukonga na baadaye nilipelekwa
Mahabusu ya Gereza la Keko, nikawa napelekwa mahakamani hadi Septemba
mwaka huo ambako nilihukumiwa kwenda jela miezi 9.
“Nilitumikia
maisha ya jela hadi Desemba 10, 2009 nikatolewa kwa msamaha wa Rais
Jakaya Kikwete. Nilikwenda kuishi kwa ndugu zangu huku wakifuatilia
sababu ya kufanyiwa vitendo hivyo bila mafanikio.
“Maisha
ya kwa ndugu hayakunifurahisha kwani hata wao walikuwa na majukumu
mengi, niliamua kuendelea na kazi zangu za sanaa pia utunzaji wa
mazingira na bustani kwa watu wakawa wananilipa fedha.
“Ndipo
nilipoamua kutafuta sehemu iliyotulia ili niweze kuishi, nikapata hapa,
ni jirani na Mlimani City. Nilichimba handaki kubwa kama unavyoliona,
kwa chini kuna kitanda ninacholalia.
“Kwa
hakika hapa sipati shida, wala kelele. Kwanza ni tulivu sana, nimefikia
hatua ya kuishi kama mnyama kutokana na mateso na bugudha nilizopata,
wengi hawajui nilipo, nipo katika pori hili kwa miaka minne
sasa,”alisema Makenge.CHANZO GPL
0 comments :
Post a Comment