Marehemu William Francis,28, enzi za uhai wake
Baadhi ya viongozi wa chama cha waendesha daladala wakiendelea kukusanja michango ya rambi rambi jana mchana
Baadhi ya madereva na makondakta wa daladala wakiwa na nyuso za hudhuni baada ya kupokea taarifa za tukio hilo.
NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO.
KATIKA hali ya
kuhuzunisha kondakta wa Hiace inayofanya safari zake Kihonda - Mjini
William Francis,28, jana mchana amegongwa na Lori na kufa papo hapo eneo
la Kihonda barabra kuu ya Morogoro-Dodoma, alipokuwa akiwavusha abiria
wake ambao ni wanafunzi wa chekechea uapande wa pili wa barabara hiyo
isiyokuwa na vituo vya kushusha na kupakia abiria.
Akihojiwa na
mwandishi wa habari hizi msemaji wa chama cha madereva na makondakta wa
daladala mkoani Morogoro Bw Kigola Pazi alisema marehemu aligongwa na
gari hilo alipokuwa akiwavusha abiri wake ambao ni madenti wa shule ya
awali 'chekechea'
"Kwa nyinyi
waandishi wa habari mtusaidia kufikisha kilio chetu kwa mamlaka husika
mwenzetu amekufa akitetea roho za abiri wake kufutia barabara ya Kihonda
kukosa vituo vya kushusha na kupakia abiri, Wille aligongwa na gari
wakati akirudi upande wa pili wa barabra baada ya kuwavusha watoto
wawili wa shule ya chekechea akisema kwa uchungu msemaji huyo wa chama hicho.
Leo asubuhi
mwandishi wa habari hizi alifika kwenye kituo kikuu cha daladala
kilichopo katikatika ya mji kasoro bahari 'Morogoro' na kushuhudia
baadhi ya madereva na makondakta wakiwa na nyuso za huzuni baada ya
kupokea taariza hizo za kifo cha ghafla cha mwenzao.
'Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake libarikiwe Amen'
Chanzo: Shekidele Blog



0 comments :
Post a Comment