.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Mzee Small alaani mtu aliyemzushia kifo chake. Asema Mungu pekee ndio anajua yeye ataishi mpaka lini


Mzee Small alaani mtu aliyemzushia kifo chake. Asema Mungu pekee ndio anajua yeye ataishi mpaka lini
Msanii mkongwe wa vichekesho Said Ngamba almaarufu kama Mzee Small, amemlaani mtu aliyetoa taarifa za uongo kuwa amefariki dunia jana usiku.

 

Akizungumza na tovuti ya Bongo5 waliomtembelea nyumbani kwake Tabata Mawenzi leo asubuhi, Small amesema alipatwa na mshituko baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu wanasambaza taarifa kuwa amefariki dunia, na kumlaani mtu aliyosambaza taarifa hizo za uongo.
“Kwanza nawashukuru (Watanzania) na nawaheshimu kunipigia simu na kumtafuta mchawi, maana yake nyinyi ndiyo mumemvumbua mchawi,nawashukuru Radio zote,Tv zote nazishukuru mimi mzima bado nipo hai” Alisema Mzee huyo mcheshi.
“Kwanza mke wangu alishituka alafu mimi mwenyewe nilikuwa nimelala, lakini kwakweli mimi nilijisikia vibaya, namalaani huyo mtu,namlaani kwanzia leo mpaka kiama na mwenyezi mungu atamuona na kumsikia” Alisema Mzee Small.
Naye mke wa Mzee Small amesema kwa upande wake ameathirika kwa kiasi fulani kwakuwa yeye ni muuguzi mkuu, alihitaji kuulizwa maendeleo ya Mzee Small kabla ya kutangaza taarifa za uongo.
“Mimi ni mke wa Mzee Small kwakweli kwa tukio lililotokea limeniumiza sana kwasababu mimi ndiyo muuguzaji mkuu wa huyu bwana,niko nae inakuwa vigumu jambo kama hili linapotokea wakati mimi sijui chochote, kwakweli limeniumiza. Nawaomba Watanzania tufike mahala tuangalie, tusianze kusambaza vitu ambavyo hatuka ukweli navyo” Alisema mke wa Small.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad