WAKATI takwimu za ongezeko la ukuaji wa sanaa ya muziki wa kizazi kipya nchini zikipanda huku kazi za wasanii wengi zikianza kukubalika kimataifa, mwaka 2013 umekuwa wenye mafanikio makubwa kwa baadhi ya wasanii nchini. Angalau wameweza kuvuna mkwanja mkubwa kupitia muziki wao.
Hii inatukumbusha miaka 20 iliyopita wakati
harakati za kuzaliwa kwa muziki huo zilipoanza kwa kuwahusisha
wanamuziki kadhaa akiwamo Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ wakati huo, sasa
‘Sugu’.
Mwaka 2013 pia umekuwa wa neema kwani kumekuwa na
ongezeko kubwa la malipo ya shoo yaliyowawezesha wasanii wengi kujikimu
kimaisha na kufanya mambo ya maendeleo.
Wengi wamejenga nyumba, wamenunua mashamba pamoja na kutimiza malengo yao, achilia mbali kununua magari.
Ingawaje miaka ya nyuma wasanii walipata ujira wa
kuanzia Sh1 milioni, katika baadhi ya matamasha mwaka huu, wasanii
walilipwa kuanzia Sh3 milioni kwenda juu.
Wakati neema hizo zikiendelea, wasanii wengi
walitoa vibao vyao kadhaa ambavyo zaidi yake vipo vilivyoweza kubamba
zaidi na kukamata nafasi za juu.
Kuanzia Januari mpaka mwanzoni mwa Desemba, wapo
wanamuziki 10 walioweza kufanya vizuri na kazi zao kutamba sokoni
sambamba na kuangaliwa na idadi kubwa ya mashabiki ndani na nje ya
Tanzania kupitia mtandao maarufu You Tube.
Nyimbo hizi ndizo zilizohusika kwa kiwango kikubwa
kuwatafutia mastaa hawa shoo za maana na zenye malipo makubwa. Ndani ya
vibao hivi vilivyotamba ndiko wanakozaliwa wasanii waliofanya vizuri
kwa mwaka kulingana na kazi zao walizozitoa kwa kipindi cha miezi 12.
My Number One (Diamond)
Video ya wimbo huu imepata watazamaji zaidi ya 1.5
milioni tangu ulipowekwa You Tube kwa mara ya kwanza mwezi Septemba. Ni
wimbo ulioweza kumtambulisha Diamond kimataifa.
Alirekodi katika studio ya kawaida sana, Burn Records, lakini wimbo huo umeweza kumkutanisha na mastaa wakubwa barani Afrika.
Kwa mara ya kwanza ameweza kufanya kolabo na
Davido, Iyanya na wanamuziki wengine mashuhuri barani Afrika. Ameweza
kutambulika kimataifa kutokana na video hiyo kuonyeshwa katika
televisheni nyingi Afrika sambamba na mahojiano.
Tupogo (Ommy Dimpoz)
Cheza Bila Kukunja Goti
Muziki Gani
Yahaya (Lady Jaydee)
Majanga (Snura)
Roho Yangu (Rich Mavoko)
Dear Gambe (Young Killer)
Ni wimbo wa mwanamuziki chipukizi, Young Killer.
Huyu ameweza kutamba na vibao vingine pia kikiwamo ‘Mrs Super Star’,
lakini Dear Gambe ndiyo umeoongoza katika vibao vyake.
Amepata shoo nyingi, ni kijana mdogo aliyeibukia
katika Super Nyota 2012. Ameweza kuliteka soko na kupata shoo nyingi
zilizomwingizia kipato kikubwa.
Tupogo (Ommy Dimpoz)
Ni wimbo uliowakusanya wanamuziki kadhaa akiwamo
J. Martin na vionjo vimewekwa na Mafumu Bilali. Shoo alizozipata Ommy
Dimpoz mwaka huu zimechangiwa mno na wimbo huu kipenzi cha wengi.
Ni wimbo unaoelezea upendo na kudumu katika mapenzi, umekuwa kipaumbele hata kwenye harusi nyingi.
Cheza Bila Kukunja Goti
(Mwana FA & AY)
Hapa tunamkuta tena Mafumu Bilali akiwa na
tarumbeta lake. Yeye ndiye aliyeweza kuunogesha zaidi wimbo huu kwa
kuongeza vionjo kadha wa kadha.
Ni kati ya nyimbo chache zilizofanikiwa kutumiwa katika huduma muhimu za kwenye mitandao ya kijamii.
Ukimpigia mtu simu na usipompata hewani, unasindikizwa na wimbo huu huku ukipewa ujumbe kwamba mtu uliyempigia hapatikani.
Muziki Gani
(Ney Wa Mitego, Diamond)
Ni wimbo wenye vionjo vya aina yake. Mistari
iliyoimbwa ndani ya wimbo huo iliwafanya wengi wahoji uhalali wa Ney Wa
Mitego kuwasema wabana pua, hali kadhalika Diamond kuwasema Hip Hop
kwamba wanatoboa pua.
Ni kolabo iliyoweza kuwaletea umaarufu mkubwa
wasanii hao hasa pale walipoimba pamoja katika Ukumbi wa Dar Live na
kuteka idadi kubwa ya mashabiki. Unapendwa na wengi.
Yahaya (Lady Jaydee)
Kwa kipindi kirefu kiasi, Judith Wambura, alikuwa
kimya kidogo na hata alipotoa wimbo hakutingisha sana. Lakini alipotoa
‘Yahaya’ alitingisha.
Ni wimbo uliojizolea umaarufu na ndiyo ulioimbwa
pia na mwigizaji wa filamu, Lulu, siku ya uzinduzi wa filamu ya ‘Foolish
Age’. Yahaya pia ulimjazia Lady Jaydee mashabiki katika shoo yake ya
miaka 13 ya Lady Jay Dee katika muziki.
Majanga (Snura)
Ni wimbo uliomtambulisha Snura katika ramani ya
muziki akitokea katika uigizaji. Japokuwa Majanga aliiuachia mwaka 2012,
lakini ulishika chati zaidi mwaka huu.
Kwa wimbo huo mmoja tu, ameweza kupata shoo zaidi
ya 60 ambazo zimemwingizia kipato kikubwa ukilinganisha na
alipojihusisha na uigizaji.
Majanga ni wimbo uliokuja wakati mwafaka kwani
maudhui yake yalifanana na matukio yaliyokuwa yakitokea miongoni mwa
jamii na hivyo kuwafanya watu kutunga msemo wa majanga wakisemea kitu
kibaya au chenye kustaajabisha.
Roho Yangu (Rich Mavoko)
Ingawa wimbo huu bado haujaonyesha takwimu halisi
ya shoo alizozifanya Rich Mavoko, lakini umetoa changamoto kwa wasanii
wengine nchini ambao hawakuwahi kudhani kama msanii huyu ana uwezo
mkubwa kimuziki.
Salamu Zao (Ney Wa Mitego)
Utamu (Dully Sykes)
Ndani ya mashairi yake, ameikumbusha jamii kwamba kitanda
hakizai haramu lakini akimwachia msikilizaji maswali. Ni njia mojawapo
ya mafanikio, kwani mpaka msikilizaji apate jawabu, tayari ujumbe
unakuwa umefika.
Salamu Zao (Ney Wa Mitego)
Ni wimbo uliozua mtafaruku mkubwa miongoni mwa
mastaa, lakini ulioelezea ukweli na kuleta mabadiliko makubwa miongoni
mwa maeneo ambayo ameyagusa.
Mara zote Ney wa Mitego amekuwa akizungumza mambo moja kwa moja katika ngoma zake na katika sehemu ya wimbo huo anaimba;
‘’...Hizi Salamu ziende kwa Madam Rita na Bongo
Star Search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi? Namuona Walter
Chilambo kapigika kama zamani, Haji Ramadhani kachoka yupo
kitaani...Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji
wekeni mambo hadharani...”
Utamu (Dully Sykes)
Amewashirikisha Ommy Dimpoz na Diamond. Umepambwa
zaidi na matarumbeta ya Mafumu Bilali. Ni kati ya nyimbo zilizofanya
vizuri mwaka 2013 kwa kuangaliwa pia kwenye You Tube, pia umetamba
katika miito ya simu zao za mkononi.
0 comments :
Post a Comment