JUZI Alhamisi usiku, Nelson Mandela ambaye ni Rais wa zamani wa Afrika Kusini alifariki Dunia nyumbani kwake Johannesburg baada ya kupambana kwa muda mrefu na ugonjwa wa mapafu.
Ugonjwa huo ulimsumbua sana kiasi cha kusababisha apelekwe hospitali mara nne katika kipindi cha miezi tisa ya hivi karibuni.
Kifo chake kimetokea akiwa na umri wa miaka 95 na
kuwaachia majonzi makubwa watu wa Afrika Kusini na Dunia kwa ujumla
wakiomboleza msiba huo mkubwa.
Kupambana na kuifanikisha Afrika Kusini kuandaa
fainali za Kombe la Dunia 2010 ilikuwa ni moja ya mapenzi ya kiongozi
huyo katika michezo ukiweka kando historia yake kwamba alikuwa bondia wa
ridhaa enzi zake za ujana.
Mpenzi wa soka
Jitihada na mapenzi yake kwenye mchezo wa soka
yalikuwa sababu kubwa ya fainali za Kombe la Dunia kufanyika Afrika
Kusini, ikiwa ni mara ya kwanza fainali hizo kuchezwa kwenye ardhi ya
Bara la Afrika tangu zilipoanzishwa mwaka 1930.
Katika juhudi zake za kuondoa ubaguzi, Mandela
alitumia michezo kuunganisha nchi hiyo, ambapo alisababisha kufanyika
kwa fainali za Kombe la Dunia la mchezo wa rugby nchini humo mwaka 1995
na fainali za soka za Mataifa ya Afrika mwaka 1996.
Baada ya kufanikiwa kwa michuano hiyo, Mandela
aliendelea kusapoti juhudi za kutumia michezo na hasa soka na hivyo nchi
hiyo kufanikiwa kuandaa michuano mingine mikubwa ikiwa fainali za soka
za Kombe la Dunia zinazoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Soka
(Fifa).
Baada ya kushindwa kupata uenyeji wa fainali hizo
mwaka 2006, miaka minne baadaye Afrika Kusini ikiongozwa na Mandela
iliweza kushinda na hivyo kupata wenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2010,
ambalo lilifanyika kwa mafanikio na Hispania kuibuka mabingwa.
Uwanja waitwa jina lake
Uwanja wa soka wa Port Elizabeth ambao ulitumika
kwa mechi nyingi kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010, ulipewa
jina la Nelson Mandela Bay na hilo limekuja baada ya kufanikiwa kwenye
kuzifanya fainali hizo kufanyika nchini humo.
Afrika Kusini inajivunia kuwahi kumpata kiongozi
ambaye hakuvunjika moyo kutokana na kufungwa jela au mateso aliyoyapata
katika harakati za kisiasa, badala yake alikuwa mtu mwenye kuhamasisha
umoja na amani jambo ambalo limempa heshima kubwa duniani kote.
Yaya Toure amlilia
Ronaldo, Blatter waomboleza
Pique, Adebayor wamlilia
Wanasoka mbalimbali duniani kote wameguswa na kifo cha kiongozi
huyo, aliyeiwezesha Afrika kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia,
lakini akiwa amekufa siku moja kabla ya kufanyika kwa droo ya makundi ya
fainali nyingine za Kombe la Dunia za mwakani zitakazochezwa Brazil.
Yaya Toure amlilia
Kiungo wa Ivory Coast na Manchester City, Yaya
Toure, hakusita kuonyesha kuguswa na msiba wa Mandela na kuweka ujumbe
maalumu katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter uliosomeka hivi:
“Shujaa ni mtu ambaye anajitolea maisha yake kwa ajili ya manufaa
makubwa bila ya kujijali mwenyewe atapatwa na kitu gani.
Dunia imepoteza shujaa na Afrika imepoteza baba...RIP Mandela.”
Pienaar haamini, Pele anena
Taarifa za kifo cha Mandela zimemshitua kiungo wa
Afrika Kusini, Steven Pienaar na kusema kwamba haamini kama ripoti hizo
ni za kweli kama Madiba amefariki Dunia.
Wakati Pienaar akishikwa na kigugumizi juu ya
taarifa hizo, gwiji la Brazil, Pele alisema kwa sasa ni wakati mwafaka
wa kuendeleza yale mazuri yake kwa vitendo ili kuendelea kumkumbuka
kiongozi huyo kwa ushujaa wake.
Ronaldo, Blatter waomboleza
Kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010,
Cristiano Ronaldo alikutana na Mandela na kumpelekea jezi ya timu ya
taifa ya Ureno iliyokuwa na Namba 16. Kwa dakika chache aliketi pamoja
na kiongozi huyo na kupiga picha naye, Ronaldo amevuna vitu vingi na
hivyo alionyeshwa kuguswa kwake kwa kifo hicho na kumshukuru Mandela kwa
ushujaa wake na kuwa mfano bora.
Rais wa Fifa, Sepp Blatter, aliungana na jamii
nyingine kutoka kwenye familia ya mchezo wa soka kutoa rambirambi kwa
kiongozi huyo na kusema daima ataendelea kuheshimu jitihada za Mandela
ambaye atabaki kuwa mpambanaji wa haki za binadamu katika kizazi chake.
Pique, Adebayor wamlilia
Beki wa Barcelona, Mhispaniola Gerard Pique,
anasema fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 zitabaki kwenye
kumbukumbu zake daima na hii si kwa sababu nchi yake ya Hispania
ilinyakua ubingwa, bali ni jinsi Mandela alivyoweza kufanya kitu hicho
kutokea na kufanyika kwa mafanikio makubwa kwenye ardhi ya Afrika.
Kompany, Gyan na Bassong nao wamlilia
Carrick, Ayew wamzungumzia
Usichokijua
Wakati Pique akimshukuru Mandela kwa hilo, straika wa Togo na
Tottenham Hotspurs, Emmanuel Abedayor, ambaye aliwahi kukutana ana kwa
ana na kiongozi huyo, alisema hakika Mandela atabaki kuwa kiongozi bora
wa nyakati zote kutokana na ujasiri wake na uhamasishaji na kwamba
ameacha sifa ambayo itadumu karne kwa karne.
Kompany, Gyan na Bassong nao wamlilia
Kwenye taarifa yake, nahodha wa Manchester City,
Mbelgiji Vincent Kompany, alisema moja ya mambo anayoyapenda kwenye
maisha yake ni kusoma vitabu vinavyomhusu Mandela na jinsi alivyoikomboa
Afrika Kusini.
Baada ya kupata taarifa za kifo cha kiongozi huyo,
Kompany anakiri kuishiwa maneno yanayofaa kumzungumzia Mandela hasa
kutokana na mambo aliyoifanyia Dunia na kuwa mfano mkubwa.
Beki Sebastien Bassong amesema daima ataendeleza
mapenzi yake kwa Madiba na kwamba kiongozi huyo ni mmoja wa mashujaa
wake kwenye maisha.
Straika wa Ghana, Asamoah Gyan, anaeleza furaha ya
kuwahi kukutana na Mandela na kusema jambo hilo hakika litabaki kuwa la
kipekee kabisa kwake huku akimtakia mapumziko ya amani.
Carrick, Ayew wamzungumzia
Kiungo Mwingereza wa Manchester United, Michael
Carrick amemzungumzia Mandela na kusema moja ya hazina kubwa iliyowahi
kutokea duniani na kwamba maisha yake yamekatika, lakini heshima yake
itabaki daima.
Naye straika wa Ghana na Olympique Marseille,
Andre Ayew, anaamini Madiba ni mtu makini zaidi aliyewahi kutokea
duniani na hasa kwenye bara la Afrika.
Straika wa Tottenham Hotspura na England, Jermain
Defoe, alipokea taarifa za kifo hicho cha Mandela akiwa kwenye ukumbi wa
sinema kutika uzinduzi wa filamu inayohusu maisha ya kiongozi huyo wa
Afrika Kusini.
Usichokijua
Wengi wameanza kumfahamu akiwa tayari mzee, mvi
kichwani na tayari ameanza kuchoka. Hii ni kwa sababu tu, tayari alikuwa
na umri wa miaka 71 macho ya wengi yalipoanza kumtambua kwa kuwa ndiyo
kwanza alikuwa anatoka jela mwaka 1990.
Akizaliwa katika familia yenye hadhi ya kifalme kijijini Transkei
Historia fupi
Lakini, kwenye ujana wake, Nelson Mandela, alikuwa mwenye kimo
kirefu, mwili uliojengeka vizuri, bondia na dansa ambaye marafiki zake
walikiri kwamba alikuwa kivutio cha mabinti warembo.
Akizaliwa katika familia yenye hadhi ya kifalme kijijini Transkei
Mandela alikuwa mchangamfu na mwenye kujiamini.
Maisha ya kifalme si kitu alichokitaka, baada ya kugundua mpango wa
kumtaka aoe mara tu atakapomaliza shule, aliamua kutoroka na kukimbilia
Alexandra, mji wa watu weusi uliokuwa nje kidogo ya Johannesburg.
Kama ilivyo kwa wanaume wote wa umri wake, mwenye
afya alijihusisha na maisha ya wanawake na kwa sababu alikuwa mjini,
basi haikuwa tabu kuwapata.
Akifanya kazi kama karani wa mahakama, akihitaji
sheria nyakati za usiku kwa lengo la kutaka kuwa mkombozi wa taifa lake,
Mandela alipanga katika nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na Evelyn Mase,
nesi mrembo aliyekuwa binti mdogo kipindi hicho.
Evelyn kwa mdomo wake alikiri kumpenda Mandela
siku ya kwanza tu baada ya kukutana, kipindi hicho Mandela akiwa na umri
wa miaka 26, alimchumbia mrembo Evelyn aliyekuwa na umri wa miaka 23 na
wawili hao walioana Johannesburg .
Historia fupi
Mandela alizaliwa Julai 18, 1918 kijijini Mvezo,
Umtatu, ambayo baadaye ikawa sehemu ya Cape Province. Alipewa jina la
Rolihlahla, neno la Xhosa lenye maana ya “msumbufu” kabla ya kutambulika
kwa jina la ubini wake, Madiba.
Babu yake aliitwa Ngubengcuka, mtawala wa jamii ya
watu wa Thembu. Alikuwa mmoja wa watoto wa mfalme, aliyeitwa Mandela na
hiyo ndiyo chanzo cha jina la ubini wake. Kwa sababu Mandela alikuwa ni
mtoto pekee wa mfalme kutoka kwa mkewe wa jamii ya Ixhiba.
Baba yake, Gadla Henry Mphakanyiswa, alikuwa chifu. Mwaka 1926, Gadla, alitumuliwa kazi kwa rushwa
Gadla alikuwa mume wa mitara. Alikuwa na wanawake
wanne, watoto wanne wa kiume na tisa wa kike, waliokuwa wakiishi vijiji
tofauti.
Mama yake Mandela alikuwa ni mke wa tatu wa Gadla,
Nosekeni Fanny, aliyekuwa binti wa Nkedama kutoka jamii ya Mpemvu
kutoka koo za Xhosa.
Pumzika kwa amani Madiba.
credit to Mwanaspoti....
Pumzika kwa amani Madiba.
credit to Mwanaspoti....
0 comments :
Post a Comment