Mshambuliaji mstaafu mwenye uraia wa kifaransa (Thiery Henry) aliyekuwa akiichezea club ya Arsenal iliopo kaskazini mwa jiji la London amesema kuwa timu hiyo itatwaa ubingwa wa ligi kuu ya uingereza mwaka huu.
Thiery Henry amesema kuwa anaamini kuwa kocha wa timu hiyo amebadilisha falsafa ya mpira katika club hiyo kwa silimia kubwa sana hivyo ni lazima Arsenal itatwaa ubingwa wa ligi ya uingereza msimu huu.
Mshambuliaji huyo msaafu wa ufaransa aliifungia club ya Arsenal jumla ya magoli 226 katika michezo 369 aliyocheza katikati ya kipindi cha mwaka 1999 mpaka 2007, kabla ya kujiunga tena kwa mara ya pili kwa mkopo uliosainiwa wa kuitumikia tena arsenal kwa miezi miwili mnamo mwaka 2012 akitokea club ya New York Red Bulls, ambayo bado hanaichezea mpaka sasa.
Henry ameshinda mataji saba akiwa na washika bunduki hao wa kaskasnini mwa jiji la London, lakini toka mwaka 2005 mpaka sasa Arsenal haijafanikiwa kunyakua taji lolote lile la dhahabu. Chanzo, goal.com (R.M)
Ikumbukwe kuwa arsenal mpaka sasa ndio wababe wa ligi hiyo katika michezo yote 21 waliyoicheza hivyo Henry alisisitiza kuwa ana uhakika kuwa Arsenal watatetea ubingwa huo.
Anasema, '' mara nyingi nawaangalia Arsenal'', alisema hayo katika tukio moja huko Barcelona pia alisisitiza, '' wameanza vizuri msimu huu. ni matuamini yangu kuwa watazidisha uwezo, na pia watatwaa ubingwa huo.
Henry alitoa shukhrani zake za pongezi kwa meneja wa timu hiyo, aliyemsajili kutoka club ya Juventus mnamo mwaka 1999 kuwa amebadilisha falsafa ya timu hiyo kwa asilimia kubwa.
Mshabuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alisema kuwa, '' Wenger amebadilisha falsafa ya mpira wa Arsenal''. pia mapema alivyowasili katika club hiyo alitwaa tuzo, hivyo kuweza kukubalika, kuaminiwa pia kueshimiwa na kila mtu.
Mshambuliaji huyo aliondoka katika club ya Arsenal mnamo mwaka 2007 na kujiunga na club ya Barcelona, ambapo aliweza kushinda mataji matatu katika kipindi cha mwaka 2008 mpaka 2009 chini ya Pep Guardiola.
Pia alisisitiza kuwa anaamini club hiyo ya wacatalan ipo katika usawa mzuri, chini ya meneja mwenye uraia wa argentine, Gerardo Martino.
Aliulizwa ''hadi sasa Barcelona ina point ngapi ''? akajibu,'' sidhani kama point 50 ni mbaya (katika La Liga) wamebadilisha kocha kipindi cha joto lakini kila nikiwaona, wanacheza vizuri pia – ni timu kubwa na nzuri, alisema Henry, 36.
0 comments :
Post a Comment