.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Ramadhan Singano ‘Messi’ ondoka Simba


MAKOCHA wa Simba, Zradvko Logarusic na msaidizi wake Selemani Matola ambaye ni Baba mlezi wa soka wa Ramadhani Singano ‘Messi’, hawakumpa nafasi ya kwanza mwanasoka huyo katika mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga iliyochezwa Desemba 21 mwaka jana.
Huenda hawakumwandaa kucheza au hawakumwamini, ni tofauti na ilivyokuwa kwa Said Ndemla aliyeanza. Hata hivyo, ni kwamba Singano alikuwa katika kiwango cha juu mno cha uchezaji wake siku hiyo kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa wana wa Jangwani.
Singano ameleta mtafaruku mkubwa pale Jangwani, Sasa kocha, Ernest Brandts, ambaye hivi karibuni mkataba wake uliongezwa muda wa mwaka mmoja, keshapewa notisi. Masikini Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wako kikaangoni, eti walicheza chini ya kiwango.
Watu wanasahau kuwa Singano alikuwa katika kiwango chake cha mwisho kabisa cha ubora, kinachotakiwa sasa kwake ni kutafuta malisho mengine kulingana na umri wake ulivyo.
Yondani na Cannavaro hawana makosa hata kidogo, umri wao unawaruhusu kabisa kucheza walivyocheza mbele ya dogo Singano mwenye umri usiozidi miaka 21.
Nitashangaa nikimkuta Singano akiwa Mtaa wa Samora akitafuta kununua TV kubwa na redio ya kisasa, nitafadhaika nikimwona Singano na wapambe wake wakitafuta kiwanja maeneo ya Chamazi, Mbande au Tuangoma, inaniuma mno nikisikia watu wanamsifia Singano eti ana akili kisa kanunua gari la biashara kalipaki pale Buguruni.
Natamani niwe mshauri wake sasa, natamani ningekuwa wakala wa wachezaji kama alivyo rafiki yangu, Damas Ndumbalo. Ningekuwa hivyo nisingemwacha Singano hivi hivi, ningehakikisha namuuza Ulaya.
Singano ana kila kitu katika soka cha kumfanya asajiliwe Ulaya, kama kuna kitu anachopungukiwa nacho ni nguvu tu. Ili Singano aingie kwenye soka la ushindani, ni lazima aachane na biashara ya kununua TV, redio au kiwanja. Ni lazima apigane na kula, ni lazima afikie hatua ya kuweza kula kuku wa kinyeji wawili na kunywa lita mbili za maji kwa wakati mmoja.
Singano atakapofikia malengo ya kupambana na Wazungu katika baridi kali, mahali ambapo soka linalipa, nafasi ya kununua kiwanja itakuwa haipo tena atakuja kununua mtaa mzima pale Masaki. Hivyo ndiyo soka lilivyo.
Katika moja ya makala zangu, niliwahi kumwambia Mbwana Samatta aende Simba, aifanye klabu hiyo njia na sasa wanaomwona Samatta hawana la kusema. Wenye macho ya kuona mbali tumekuona Singano, Simba na Tanzania kwa ujumla si mahala pako, ondoka katafute malisho mengine.
Damas Ndumbalo, Salehe Ally wa Zanzibar, Saidi Tully sifa yenu nyie ni mawakala. Hivi kweli hamjamwona Singano? Au macho yangu siku hizi ni ya makengeza?
Naamini ni wakati wenu sasa wa kumtamfutia mtu maalumu au watu maalumu wa kumwandaa Singano kimazoezi, kiafya na kisaikolojia ili awe Singano anayestahili. Kwa sasa anatakiwa aishi maisha ya kuvuna kulingana na kazi yake, maisha ya kutoka jasho la damu ili muda mfupi ujao dunia imtambue.

Ni jukumu lenu kumwandaa, kumuachanisha na matajiri uchwara wa nchini ambao siku zote kwao ni fahari kuwahodhi wachezaji wazuri kujilinda na migogoro kwenye klabu zao, lakini mwishowe wanawatupa.
Ni jukumu lenu akina Ndumalo kumwelekeza kijana huyo awaangalie akina Haruna Moshi ‘Boban’, Athuman Idd ‘Chuji’, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa jinsi walivyopoteza dira. Miguu yao imejaa utajiri kwa soka walilojaaliwa, lakini wanaishia hapa hapa bila ya kuwa na mavuno makubwa.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad