Mlevi mmoja huko Uingereza ambae ni shabiki wa Manchester United amepiga
simu 999 akiagiza kwamba anataka kuongea na kocha aliepita ambae ni Sir
Alex Ferguson kuhusu matokeo ya mechi baada ya club hii kutolewa
Capital One cup.
Huyu shabiki akiwa na uchungu aliwapigia simu polisi ambao wapo
kaskazini mwa mji huo muda mfupi tu baada ya Red Devil’s kushindwa na
kutolewa na Sunderland kwa mikwaju.
Polisi wa Greater Manchester walitoa tamko wakisema “Jana usiku saa nne
na nusu mwanaume mmoja kutoka maeneo ya Crumpsall kaskazini mwa
Manchester alipiga simu 999 akiwa na sauti ya mtu aliyelewa akiamuru
koungea na Sir Alex kuhusu matokeo ya mechi, ni kawaida kuwa na machungu
pale timu yako inaposhindwa lakini tukumbuke namba 999 ni kwa ajili ya
huduma za dharura tu kwa raia ndio maana kwa visivyo vya dharura namba
101 ndio inatumika’
0 comments :
Post a Comment