JEZI ya Mbeya City ndiyo ya gharama kuliko zile za wakongwe Simba na Yanga, hii ni kwa mujibu wa mauzo ya mitaani.
Ukitaka jezi halisi ya Mbeya City utalazimika
kulipa zaidi ya Sh15,000 ukiwa nje ya jiji la Mbeya, kwani jijini humo
inapatikana kwa gharama hiyo katika duka lao.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mbeya City, Fred
Jackson, jezi zao wanaziuza kwa bei ya Sh15,000 lakini hadi ikifika Dar
es Salaam au mkoa mwingne wowote inaweza kugharimu hadi Sh25,000.
“Wapo wanaouza jezi zetu hadi Sh35,000,
tumewakataza wasiuze kwa bei ya juu kiasi hicho, kwani wanawaumiza
wananchi. Tuna tawi pale Ubungo Terminal (kituo cha mabasi ya mikoani
cha Dar es Salaam) na huwa tunazipeleka huko,” alisema Fred.
Hata hivyo Mwanaspoti limeshuhudia jezi hizo
halisi za Mbeya City zenye nembo ya timu zikiuzwa kwa Sh25,000 huku zile
ambazo si halali zikiuzwa kwa Sh15,000.
Jezi za Simba, Azam na Yanga ambazo si halisi
zenyewe zinauzwa kwa Sh10,000. Bado hakuna jezi halisi za Simba na Yanga
zinazouzwa madukani au mitaani.
Tangu Mbeya City ilipoanza kwa kishindo Ligi Kuu
Bara msimu huu ambao ndio wa kwanza kwao, jezi za timu hiyo zimegeuka
dili ambapo mashabiki mbalimbali wamekuwa wakizinunua kwa wingi. Hata
hivyo hali hiyo imetoa mwanya kwa wajanja kutengeneza jezi hizo na
kuziuza kwa Sh15,000 zikiwa hazina nembo ya timu hiyo.
0 comments :
Post a Comment