KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema ni miujiza tu ndiyo inayoweza kuifanya timu hiyo ichukue ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwani mambo yamezidi kuwa magumu ingawa hawakati tamaa na watapambana mpaka mwisho kujua wako nafasi ipi.
Simba ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 32, nne
nyuma ya vinara wa ligi hiyo Azam wenye pointi 36 huku Yanga ikiwa ya
pili kwa kuwa na pointi 35 sawa na Mbeya City.
Lakini licha ya timu hiyo kuwa nyuma ya wapinzani
wao kwa pointi hizo, pia imecheza mechi nyingi zaidi ya Yanga na Azam.
Simba imecheza michezo 18 wakati Yanga na Azam zimecheza michezo 16
hivyo zina mechi mbili mkononi.
Timu hiyo imeambulia pointi mbili tu katika mechi
zake tatu ilizocheza mikoani na imebakiza mechi mbili za nje ya Dar es
Salaam dhidi ya Prisons Machi 3 na Kagera Sugar Machi 30.
Logarusic alisema: “Ligi ni ngumu sana na
ukiangalia matokeo yetu ya hivi karibuni yanazidi kutuweka mahali
pabaya, hivyo ni muhimu kumuomba Mungu. Tunahitaji miujiza ili tupate
nafasi mbili za juu ingawa si jambo rahisi, lakini kwenye soka lolote
linaweza kutokea.
“Wapinzani wetu kuna mechi mbili bado hawajacheza
ili twende sawa na hujui mechi hizo zitakuaje, kama wakishinda basi ndio
tutazidi kupotea, lakini kama watapoteza baadhi ya mechi na sisi
tukishinda mechi zetu zinazofuata, tunaweza kujipa matumaini.
“Wachezaji wangu wanatakiwa kupambana hadi dakika ya mwisho na mwisho wa ligi tutajua tuko katika nafasi gani.”
0 comments :
Post a Comment