.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

LULU ATINGA MAHAKAMANI, KESI YAAIRISHWA.









Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabiri muigizaji wa kike, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu imesikilizwa leo (February 17) katika mahakama kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
 
Lulu alikiri mbele ya Jaji Rose Temba kuwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu Steven Kanumba na kwamba walikuwa na ugomvi, lakini alikana mashitaka ya kumuua bila kukusudia.
 
Mbali na kukiri kuwa na uhusianano wa mapenzi, muigizaji huyo pia alikiri kuwa baada ya tukio hilo alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia mdogo wake marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa Kanumba ametangulia mbele ya haki.
 
Akisoma hati ya mashitaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo, alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam, mshitakiwa alimuua bila kukusudia Stevin Kanumba.
 
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba baada ya kufa, mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya ubongo.
 
Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi pia unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.
source: Jestina george blog
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad