Maafisa wa Polisi wakisaidia abiria kutoka kwenye ndege hiyo ya shirika la ndege la Ethiopia iliyokuwa imetekwa.
Rubani msaidizi wa ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia iliyokuwa ikielekea Roma, Italia aliteka ndege hiyo Jumatatu na kutuia salama Geneva ambako alikamatwa.
Maafisa wanasema rubani huyo ambaye jina lake halikutajwa ana umri wa miaka thelathini. Alichukua udhibiti wa ndege hiyo ya 767 kwa kufunga mlango wa rubani baada ya rubani kutoka kuelekea kujisaidia.
Maafisa wa Uswisi wanasema mara ndege hiyo ilipotua Geneva rubani huyo msaidizi alitoka kwenye ndege hiyo kwa kutumia kamba na kujisalimisha kwa maafisa na kusema kwamba alikuwa ni 'haramia' anayetafuta hifadhi ya kisiasa kwa sababu alikuwa akiogopa kuteswa nyumbani .
Chanzo cha mateso hayo hakijafahamika mara moja.Ndege hiyo ilitokea mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa na ilikuwa imebeba abiria 202.
Chanzo, voaswahili.com
0 comments :
Post a Comment