Mtu
mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Bahati maarufu kwa uuzaji wa
mifuko ya plastiki maeneo ya stand kuu ya mabasi Bukoba amekutwa
kajinyonga juu ya mti maeneo ya ufukwe wa Spice Motel majira ya saa
nane mchana ..
Taarifa
za awali kutoka kwa watu waliokuwa katika tukio hilo zinasema kuwa ,
kabla ya kifo cha, marehemu alionekana akiwa na mafurushi ya vitu na
alikuwa akifua katika eneo hilo la ufukwe...
Mtu mmoja
ambae hakuwa tayari kutaja jina lake ameueleza mtandao huu kuwa
leo majira ya saa 12.00asubuhi alisalimiana na marehemu maeneo ya stand
ya mabasi akiendelea na shughuli yake ya kutembeza mifuko ya plastiki
kwenye mabasi yaendayo mikoani na maeneo mengine akiwa mzima wa afya.
Mwili wa marehemu umepelekwa Hospital ya Mkoa wa Kagera kuifadhiwa kwa ajili ya utambuzi ( ndugu zake )
Amekutwa katika hali hii
Haijafahamika ni kwa nini kachukua maamuzi haya
Mwili wa marehemu ukishushwa
Kamanda wa polisi wilaya ya Bukoba akishuhudia tukio
Wananchi waliokusanyika katika tukio
Mkuu wa kituo cha polisi Bukoba(mwenye koti) akiwa anaangalia baadhi uya vitu vya marehemu alivyokuja navyo kabla ya kujinyonga
Hivi ni vitu vya marehemu alivyokuja navyo babla ya kujinyonga
Maeneo ya spice beach
Mmoja wa watu wa kwanza kutoa taarifa kituo cha polisi Mama Faima
0 comments :
Post a Comment