.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Ajabu ya Mwaka!!!!!!!!!!!! Chatu apambana na Mamba na hatimaye kumshinda nguvu na kumla huko Australia.

 
Nyoka huyo alijipindua kwa Mamba na kumbana hadi akafa
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpindua na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipindua kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.


Nyoka huyo alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji 
Chatu huyo alianza kumla Mamba na kuwashangaza wakazi wa eneo hilo!!!
Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake
Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC
"tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumpindua mamba na kumzungusha hasa katika sehemu ya miguu yake ili kumdhibiti.''
"pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kunza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua Nyoka dakika kumi na tano kumla yule Mamba.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu masaa 5. Hatimaye wote walionekana kuchoka.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad