.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

TIMU YA BRAZIL YAMCHAPA SOUTH AFRICA MAGOLI 5.. VIDEO NA PICHA ZIPO HAPA.. "WASOUTH AFRICA WASHANGILIA KUFUNGWA NA NEYMAR"


Neymar akishangalia goli lake lakwanza katika dakika ya 41 wakiwa na jezi za kijani
"Mashabiki wa timu ya taifa ya South Africa washangilia kufungwa na Neymar" hayo ndo yalikua moja ya maneno yaliotamkwa na mmoja wa watangazaji wa pambano hilo lililofanyika huko South Africa katika kiwanja cha kimataifa ambacho kilichezewa Fainali ya kombe la Dunia mwaka 2010.

Hii ilikua ni mechi ya kirafiki ambapo Neymar aliweza kutupia magoli 3 (Hat trick) katika mechi io huku Oscar akishinda goli 1 na pia Fernandinho alishinda goli 1
Kocha wa Brazil Felipe Schorali akitoa maelekezo kwa wachezaji wake waliokua uwanjani
Katika mechi io ambayo iliweka historia ikiwa ndo mechi yakwanza Brazil kumfunga South Africa magoli 5, Pia kwenye mechi io ya kirafiki Brazil waliweza kuvaa jezi mbili tofauti , ikiwa katika kipindi cha kwanza Brazil walikua wamevaa Jezi zao za Nyumbani ambazo ni za rangi ya Kijani na nyeupe huku South afrika wakiwa wamevaa jezi zao Nyeupe. 

Oscar akishangilia goli lake lakwanza katika dakika ya 10
 katika kipindi hicho cha kwanza Oscar aliweza kuipatia Brazil goli lakwanza katika dakika ya 10, kisha Neymar kuongeza idadi ya magoli katika dakika ya 41..


Mchezaji wa South Africa Thabo Matlaba (katikati) akiwaruka Rafinha (kulia) and Fernandinho


Paulinho (kushoto)akimiliki mpira huku Dean Furman akiwa anamkaba


Neymar (Kulia) akiwa anajaribu kumtoka Andile Jali

Neymar akishangilia goli lake lapili aliloshinda sekunde 21 baada ya kipindi cha pili kuanza
Huku katika kipindi cha pili ambapo Brazil walionekana wakiwa na Jezi za rangi ya Blue huku South africa wakiwa na rangi Nyeupe waliochezea kipindi cha kwanza, ambapo katika kipindi cha pili ilimchukua Neymar sekunde 21 tu kuweza kushinda goli la 3 kwa timu yake huku yeye akiwa na magoli mawili na kisha ilipofika dakika ya 75 Fernandinho aliongeza idadi ya magoli kua 4 katika mechi kwa shuti kali alilopigia nje ya box huku akiwa amejiandikia goli lake lakwanza akiwa na kikosi cha Brazil,
 
bEKI wa South Africa Matlaba akipambana kuchukua mpira kutoka kwa Willian wa Brazil


Wachezaji wa Brazil wakishangilia pamoja na Fernadinho baada ya kufunga goli dadika ya 75


 kabla ya mpira kuisha Neymar aliweza kuongeza idadi ya magoli kua 5 katika dakika ya 90 na pia kujiandikia magoli 3 katika mechi io iliochezwa katika kiwanja cha soccer city.

ANGALIA MAGOLI HAYO HAPA 
 
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad