.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

ULISOMA HII, SAMAKI MKUBWA ATOROKA, ABURUZWA UREFU WA MAILI MOJA, APATIKANA CAR WASH

Huyu ndio Samaki Steve alietoroka kwenye mafuriko hayo
Samaki ajulikanae kwa jina la Sturgeon aliekua anahifadhiwa na kituo cha kufuga samaki  kijulikanacho kama Romsey World of Water alitoroka kutoka kwenye hifadhi yake baada ya mafuriko kutokea maeneo hayo, Samaki huyo alipatikana katika bwaawa ya kuhifadhia maji kwa ajili ya kuosha magari, sehemu hio ya kuoshea magari ijulikanayo kama Tiger Wash.

Kituo cha kuhifadhi samaki
Bwaawa analoishi samaki huyo Steve
Samaki huyo ambae alipewa jina la Steve, mwezi uliopita baada ya mafuriko kutokea katika mtoo unaopita karibu na sehemu hio ya kuhifadhi samaki, Alichukuliwa na maji yaliokua na urefu wa futi 3 na kisha kupitishwa kwenye barabara kuu na pia kuburuzwa na maji hayo na kupita pia kwenye kituo cha mafuta mpaka pale alipofika kwenye bwaawa hilo la kuhifadhi maji ya kuoshea magari.

Kituo cha kuhifadhi samaki

"Tuna mabwaawa mengi katika kituo hiki cha kuhifadhi samaki, katika mabwaawa hayo tumehifadhi samaki ambao sio wa kuhuzwa. 'Steve anaishi katika moja ya mabwaawa hayo, aitoroka na rafiki yake(samaki mkubwa tuliempa jina ya Chadwick) wakati mafuliko hayo yalipotokea." 

Na hii ndio Sheli aliopitishwa Samaki huyo wakati wa Mafuriko hayo

BaraBara kuu aliopitishwa Samaki huyo wakati wa Mafuriko hayo

"kadri wiki zilivyokua zinakwenda huku maji yakiwa yanatokomea, ndipo tulipopata simu kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa sehemu hio ya kuoshea magari ambayo ipo takribani maili moja."

Hii ndio Sehemu ya Kuoshea Magari alipopatikana Samaki Huyo

"Walisema walimuona mmoja wa samaki wetu waliopotea, walisema waliogopa samna kwa kua samaki huyo ana umbo kama la papa"

"Tunashukuru tumemkuta mzima kabisa na salama. Alikua akiishi katika bwaawa hilo la kuhifadhia maji ya kuoshea magari kwa muda wote huo" alisema Manager huyo Mr Bradbury


Huyo ni Mfanyakazi wa Car Wash hio, akiwa Pembeni ya Bwaawa hilo alipopatikana Samaki huyo

"Steve tumemkuta na mikwaruzo mingi sana, itakua alipokua anaburuzwa kwenye barabara kuu" aliongezea Mr Bradbury

Hivi sasa Samaki huo anaendelea na matibabu huku akiwa anaendelea vizuri na anaonesha amefurahi kurudi nyumbani baada ya kupatwa na mkasa huo.
Huku steve akiwa amerudi hofu ipo kwa rafiki yake ambae alitoroka nae ambae mpaka sasa hajapatikana na jitihata za kumtafuta zinaendelea,
 
Urefu wa Alisafirishwa samaki huyo

"Samaki huyo alietoroka pamoja na Steve ana urefu ya takribani miguu mitatu na uzito wa pound 25, kwa ukubwa huo tuna matumaini ya kwamba mtu atamuona na kututaarifu  " aliongeza manager huyo
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad