RAIS
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema hatajiuzulu
nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera (KRFA) pamoja na
kuwa na majukumu ya kitaifa.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa
KRFA mkoani hapa juzi Jumamosi, Malinzi alisema wakati anakuja
kuhudhuria mkutano huo alikuwa na wazo la kujiuzulu.
Hata hivyo aliwaeleza wajumbe hao kuwa ameachana na wazo la kujiuzulu
nafasi ya uenyekiti wa KRFA, kwa kuwa aliombwa na wajumbe asichukue
hatua hiyo.
Alisema baadhi ya wajumbe wa KRFA walitishia kuachia nafasi zao
endapo angejiuzulu nafasi yake ndani ya chama hicho ili aendelee
kutumikia nafasi moja ya Rais wa TFF.
Pia alisema ameamua kuendelea ili kuzima uvumi kutoka kwa wadau
mbalimbali wa soka waliodai kuwa aligombea nafasi ya uenyekiti wa KRFA
ili apate tiketi ya kugombea kiti cha urais wa TFF.
Katika hotuba yake kwa wajumbe hao Malinzi aliwataka kuhakikisha
wanashirikiana na halmashauri za wilaya ili kutenga maeneo ya viwanja
vya michezo na kusema Uwanja wa Kaitaba utawekewa nyasi bandia baada ya
kupata ufadhili wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
SOURCE: MWANASPOTI
SOURCE: MWANASPOTI
0 comments :
Post a Comment