Ni baada ya kufungwa 1-0 na West Brom Jumamosi iliyopita.Katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza Norwich iko nafasi ya nne toka chini ikiwa na pointi 32.
Ikiwa imebakiza mechi tano kumaliza mzunguko wa ligi hiyo, Norwich iko katika hati hati ya kushuka daraja na ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu yanayoweza kuibakisha katika ligi hiyo.
Katika kumalizia mzunguko wa ligi hiyo Norwich imebakisha mechi ngumu zinazoiweka katika mashaka ya kuendelea na ligi hiyo.
Mechi ilizobakiza ni kati yake na Fulham (watacheza ugenini), Liverpool (watacheza nyumbani), Man United (watacheza ugenini), Chelsea (watacheza ugenini) na Arsenal (watacheza nyumbani).
0 comments :
Post a Comment