Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe (kushoto) ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Daraja Mbili kupitia CHADEMA na Diwani wa Kata ya Levolosi, Ephata Nanyaro nae kupitia Chadema, wakisubiri kupata matibabu baada ya kupata kipigo kutoka kwa mgambo wa Jiji la Arusha leo wakati wakiwatetea Wamachinga.Kwa mujibu wa Diwani Nanyaro, anasimulia kwamba leo asubuhi alipata taarifa kuwa mgambo wa Jiji wanawapiga wananchi wafanyabiashara ndogondogo na kupora mali zao maeneo ya Kata yake, ndipo akaelekea kukutana na Naibu Meya kujionea hali halisi. Anasema alipofika alijaribu kuwasihi mgambo hao kuwa sio utaratibu kuwapiga wananchi maana hata taratibu za ukamataji haziruhusu kupiga raia.
Nanyaro
anasema wakiwa wanawashauri mgambo hao, ghafla walishangaa na yeye
amezingirwa na kuanza kupigwa sambamba na Msofe huku mgambo hao
wakiwaeleza Madiwani hao kuwa wamekuwa na kiherehere sana.
Naibu
Meya anenaAkizungumza na Blog hii Mh. Naibu Meya Prosper Msoffe
ameeleza kiini cha tatizo kuwa yeye kama kiongozi wa wananchi amekuwa
akipokea malalamiko mengi ya wananchi kupigwa, wengine kuvunjwa miguu,
mali kuporwa na mgambo, mali kifadhiwa depoti hadi kuoza. Hivyo akaamua
kufika eneo la depoti leo kujionea hali halisi na kuzungumza na mgambo
na wananchi, baada ya kufika eneo la tukio alianza kushambuliwa kwa
virungu na mateke, huku wakisema wewe umekuwa kiherehere sana na mtetezi
wa wananchi sasa tunakukomesha.
Mh.
Naibu Meya alishangazwa pia kuona kiongozi mwenzake Diwani wa Levolosi
kufika pale nae akapigwa, na kuhoji kama yeye Naibu Meya amepigwa, hali
ikoje kwa wananchi wa kawaida!??
Hatua za kisheria dhidi ya mgambo hao
0 comments :
Post a Comment