.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

PICHA YA MTOTO WA MIAKA 8 ANAETOA WATU MAPEPO NCHINI BRAZIL


Binti wa miaka nane aitwaye Alani Santos kutoka mji wa San Gonzalo nchini Brazil ameendelea kukusanya mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali nchini kwake ambao hufika kanisani anakoabudu ambako baba yake ni mchungaji ili waombewe na binti huyo anayeaminika kuwa na nguvu za ajabu za kukemea mapepo na kuponya magonjwa akitumia jina la Yesu.

Katika mji anaotokea binti huyo unaweza kufananisha na Mbeya kwa hapa Tanzania kutokana na kuwa na utitiri wa makanisa licha ya kwamba nchi hiyo kwasasa inakabiriwa na tishio la watu kutopenda masuala ya kiimani kwasasa. Brazil taifa ambalo linasifika kuwa la Kikristo wa kanisa la Katoliki, limekuwa na vipaji mbalimbali kupitia watoto akiwemo kijana Jotta A ambaye uwezo wake wa kuimba ni wa ajabu kiasi cha hata kuwashangaza waimbaji wakubwa maarufu duniani.



Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad