MATUMAINI
ya Manchester United kuwatoa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern
Munich yameingiwa doa kufuatia mshambuliaji wake tegemeo, Wayne Rooney
kuumia na ataukosa mchezo wa marudiano wa Robo Fainali wiki ijayo nchini
Ujerumani.
Rooney
aliumia Jumanne timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Old Trafford
na atafanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa maumivu yake.
Mshambuliaji
huyo England atakuwa nje katika mechi ya wikiendi hii dhidi ya
Newcastle na huku akipambana kupona acheze Jumatano Uwanja wa Allianz
Arena.
"Itakuwa
ngumu kucheza bila Wayne Jumatano," amesema kocha wa United, David
Moyes, ambaye tayari anamkosa Robin van Persie kwa wiki sita.

0 comments :
Post a Comment