![]() |
| Ndugu Chacha Makene |
CHACHA Makenge (38) aliyeripotiwa awali kuishi ndani ya handaki katika eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, amepatwa na balaa jipya baada ya makazi yake kuvamiwa na askari, kukamatwa na mwishowe kupelekwa Muhimbili kitengo cha wagonjwa wa akili kwa ajili ya matibabu.
![]() |
| Chacha akionesha mahali lilipokuwa handaki lake. |
Kana
kwamba haitoshi, Makenge ambaye aliwahi kuishi katika handaki hilo kwa
muda wa miaka mitano, alipotoka, alikuta makazi yake hayo yakiwa
yamechomwa moto na vitu vyake vyote kuchukuliwa.
kijana huyo alikiri kutokewa na mambo hayo na
kulalamika kuwa kitendo alichofanyiwa, kimempotezea mwelekeo wa maisha
yake kwani hana tena sehemu ya kwenda kwa kuwa hakujiandaa.
Alisema
alipokamatwa alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kudhaniwa kuwa
ni mgonjwa wa akili, lakini alipingana na madai hayo, licha ya kuwa
aliishi kwa siku 36 hospitalini hapo kabla ya kuruhusiwa kuondoka.
![]() |
| Chacha akifunga mlango wa handaki yalipokuwa makazi yake |




0 comments :
Post a Comment