Website ya Nairobi News imeripoti kuwa wasanii wa Afrika Mashariki wanapanga kuzisusia tuzo za MTV Africa Music Awards, MAMA.
Wasanii hao wanazishutumu tuzo hizo kwa kutozitendea haki nchini za
Afrika Mashariki mwaka huu na kwa kuwapendelea wasanii wa Afrika Kusini
na Nigeria zaidi. “Uganda imeumia zaidi kwasababu kutajwa kwao pekee ni
kwa collabo na Amani,” msanii mkubwa wa Kenya ambaye hakutaka kutajwa
jina lake aliuambia mtandao huo.
Umeandika kuwa wasanii waliotarajiwa kutajwa kwenye tuzo hizo ni AY,
Ommy Dimpoz na Lady Jaydee, Tanzania, P-Unit, STL, Elani na Wyre wa
Kenya na Jose Chameleone na Navio wa Uganda. Mtandao huo umeripoti kuwa
wasanii wengi zaidi wanapanga kutoshiriki kwenye show za utangulizi za
Road to Mamas zitakazofanyika Dar es Salaam kwa Afrika Mashariki.
0 comments :
Post a Comment