.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

BAADA YA KUTESANA STAILI YA NGOLOLO, SASA NI ZAMU YA PROKOTO,



Mwimbaji wa label ya Chocolate City, Victoria Kimani amewashirikisha Ommy Dimpoz na Diamond kwenye wimbo wake anaotarajia kuuachia May 14, unaitwa bokodo ‘Prokoto’.



Wakali hao wameutengeneza wimbo huo kwa kuunganisha lugha mbili ambazo ni Kiswahili na Kiingeza ili kutengeneza kitu ambacho kuwashika mashabiki wao kwa ujumla.

Prokoto haina maana ila ni neno tu la kutunga ambalo limetumika kama alivyozoea kufanya Dully Sykes kwenye nyimbo zake nyingi.

“Prokoto ni jina la kubuni tu ambalo itakuwa style mpya ya uchezaji, watu wataona itakavyotoka video ambayo tunatarajia kushoot very soon.” Ommy Dimpoz ameuambia mtandao huu.

Ommy Dimpoz ameeleza kuwa ‘Prokoto’ ni wimbo mkali sana wa kuchezeka ambao anaamini kwa kutumia lugha hizo mbili wimbo huo utaishika Afrika nzima.

Victoria Kimani yuko Tanzania na inawezekana akawa anaendelea na mchakato wa kushoot video ya Prokoto..
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad