.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

FIFA WATUA DAR KUWEKA NYASI BANDIA KAITABA, NYAMAGANA

MTAALAMU wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Ian McClemen amewasili nchini leo alfajiri (Mei 4 mwaka huu) ambapo atakuwepo kwa siku tatu.
McClemen ameondoka leo (Mei 4 mwak huu) kwenda Bukoba ambapo atakagua Uwanja wa Kaitaba, na kesho (Mei 5 mwaka huu) atakwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana. 
Rais wa TFF, Jamal Malinzi katikati

Viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad