KOCHA Jose Mourinho
amepigwa faini na FA ya England ya Pauni 10,000 kwa utovu wa nidhamu
baada ya kugombana na refa Mike Dean na mkuu wa marefa, Mike Riley.
Mwalimu huyo wa Chelsea, pia rufaa yake ya adhabu aliyopewa uwanja wa Villa Park Machi imetupwa, imeelezwa amekerwa na maamuzi yote hayo.
Mourinho aliwashambulia Dean na Riley mwezi uliopita kwa maneno kadhaa, baada ya Sunderland kumaliza safari yake ya kucheza mechi 78 nyumbani bila kufungwa.
FA imemkamua: Jose Mourinho ametozwa faini ya Pauni 10,000 kwa vurugu alizofanya kwenye mechi na Sunderland
Ondoka hapa: Mourinho (kulia) akimzuia Msaidizi wake, Rui Faria baada ya kutolewa nje na refa Mike Dean (kushoto

0 comments :
Post a Comment