.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

MARTIN KADINDA APANIKI BAADA YA KUSEMWA NA MPOKI KTMA 2014



Meneja wa Muigizaji maarufu wa Bongo Movie Wema sepetu amewaacha midomo wazi watu waliokuwa wamehudhuria Tuzo ya Muziki ya Kilimanjaro katika ukumbi wa mlimani City jana baada ya kupaniki na kujikuta anajibu mapigo kwa Mc wa sherehe hiyo Silvery Mjuni anayefahamika zaidi kwa jina la Mpoki.
Meneja wa Wema aitwae Martin Kadinda amejikuta ameshindwa kuzuia hisia zake kutokana na masihara ya mpoki pale alipowaambia kuwa timu Diamond ni kikundi kinachoongoza kupost picha hata zisizo na msingi kwenye mitandao ya kijamii hususani Instagram,

Mpoki aliwaambia  Diamond na wafuasi wake akiwemo Wema, Martin Kadinda,Rommy Johnson kuwa  wanapost kila wakati kwa mfano wakiwa wanakula, wamelala ndipo Martin Kadinda alipomwambia Mpoki kuwa atafute namna nyingine ya kutafutia pesa.Kauli ya Kadinda iliwashangaza wengi kwani licha ya kuwa Mpoki alikuwa anazungumza kimasihara lakini jambo lake lina ukweli kwa kiasi kikubwa japo Kadinda alikuwa mwepesi kupaniki na kushindwa kukubaliana na ukweli huo.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad