Habari zilizotapakaa kwenye mitandao mingi wikiendi iliyopita zinaeleza kuwa rapa huyo amewambia mashabiki zake kuwa baada ya tuzo za BET zitakazofanyika Jumapili ya Juni 29 mwaka huu, jina lake la kisanii litakuwa ‘Shad Moss’ jina alilopewa na wazazi wake.
”’Tangazo : Baada ya Tuzo za BET sitakuwa nikitumia tena jina la Bow Wow! nitatumia jina langu la halisi ”Shad Moss” tumeweka historia kubwa kama bow wow. Sasa ni muda wa kufungua ukurasa mpya na changamoto. Bow wow haliendani na jinsi nilivyo kwa sasa. Mimi ni baba, mfanyabiashara, mtangazaji, muigizaji na Rapa! Muda wa MR Moss kuchukua hatamu yake” alisema Bow Wow kwenye video fupi aliyoipakia(upload) kwenye ukurasa wake wa instagram.
0 comments :
Post a Comment