.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Rais wa Ghana atuma ndege yenye Pesa Brazil kuwaneemesha wachezaji



Serikali ya nchini Ghana, imetuma kiasi cha dola za kimarekani milion tatu kwa ajili ya wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo, ambayo hii leo wanakabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya timu ya taifa ya Ureno ambao utaamua kama watasonga mbele ama la, kwenye fainali za kombe la dunia zinazoendelea huko nchini Brazil.
Serikali ya Ghana ilituma fedha hizo taslim kwa njia ya ndege iliyoondoka moja kwa moja kutoka mjini Accra hadi nchini Brazil kwa amri ya raisi John Dramani Mahama, ambaye kwa sasa yupo bega kwa bega na viongozi wa chama cha soka nchini humo GFA.
Naibu waziri wa michezo nchini Ghana, Joseph Yammin, amethibitisha taarifa za kusafirishwa kwa fedha hizo kupitia kituo cha redio cha Citi FM, ambapo amesema kulikuwa na haja kubwa ya kufanya hivyo, kufuatia wachezaji kusisitiza suala la kukabidhiwa fedha taslimu na si kwa njia ya hundi.
Amesema fedha hizo ni halali kwa wachezaji, hivyo wamoena ni bora wawatumie haraka iwezekanavyo kabla hawajaingia uwanjani kupapatuana na Ureno katika mchezo ambao umebeba matumaini ya wananchi wa Ghana pamoja na mashabiki wengine wa barani Afrika.
Kabla ya hapo kulikuwa na mzozo miongoni mwa wadau wa soka nchini Ghana, kufuatia uwezo mkubwa ambao unaonyesha na wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya taifa lao, hali ambayo ilizua utata wa maswali ambayo yalihoji kwa nini wachezaji hao wasilipwe fedha zao ambazo walistahili kupewa kabla hawajaondoka.
Hata hivyo raisi wa GFA, Kwesi Nyantakyi, alijibu maswali hayo kupitia mkutano wa waandishi wa habari kwa kusema fedha hizo ni haki kwa wachezaji na zitalipwa kabla ya mchezo wa hii leo.
Sehemu ya fedha hizo pia imetolewa na raisi wa Ghana, John Dramani Mahama, baada ya kufurahishwa na uwezo na kiwango kilicho onyesha na wananchi wake wanaounda timu ya taifa analoliongoza tangu July 24 mwaka 2012.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad